MAHUBIRI N°81

MAHUBIRI JUU YA MT.24:24

(Ilihubiriwa alhamisi jioni 30 oktoba 2008 huko Anyama karibu na Abidjan– Côte d’Ivoire)



       Wandugu, Mungu awabariki. Kwanza nitajibu maswali mawili na kuzungumzia Mt.24:24 jioni ya leo. Ni wanani hao wapakwa mafuta wa uwongo na hao manabii wa uwongo katika Mt.24 :24 ? Ni wanani, wanapatikana wapi na wanafanya nini ? Ni ya muhimu sisi kuijua kwa wakati huu ya udanganyifu wa mwili na wa roho, ndiyo maana nina tamani kuizungumzia.

      Lakini kwanza, mutambue kwamba ndugu wetu Exavier alifukuzwa toka kazi yake sababu ya Kelele ya Katikati ya usiku. Alikuwa na cheo kubwa katika kampuni ya Afrika ya kusini iliyo katika jamuhuri ya kidemokratia ya Kongo na inayo simamiwa na wabranhamisti! Baadaye, ilimulazimu kuuza pikipiki yake kwa hitaji za Ujumbe!... pamoja na hayo ninamsalimu mke wake, dada Sharon na wandugu na wadada wote wa Kongo! Ndugu Exavier tayari amepita kwenye maredio nyingi za kikongomani kwa kutangaza Kelele ya Katikati ya Usiku! Ninawakumbusha kwamba yeye alikuwa muhubiri kwa wakati wa jioni! 

       Vema, ninafikia maswali. Ya kwanza ni « Ndugu Filipo, ni vipi kuhusu ndugu aliye mbali na kusanyiko na yeye ana dhambi ya kuungama …kama yeye ni katika ile ile inchi, ataungama atakapo kuwa katika kusanyiko! Kama yeye ni mgonjwa sana au yeye ni katika inchi ingine mahali hakuna kusanyiko, ataifanya kupitia mchungaji wake na mchungaji atamjulisha mpango uliyo chukuliwa na kusanyiko!

      Swali la pili ni: « Kweli kabisa kila mwafrika anaitwa kwa jina la kiafrika, sababu gani basi unaitwa tu Filipo ». Tangu kuzaliwa kwangu hadi sasa, niliitwa tu kwa jina moja: Filipo! Nilipangwa jina lingine na likawekwa juu ya kitambulisho changu lakini baba yangu aliivuta! Mimi sina haki ya kubadili jina langu lakini ni Mungu na yeye ndio wana ile haki! Watoto wote wa baba yangu wanaitwa kwa jina la kiafrika ila tu mimi! Baba yangu, mama yangu, ndugu zangu na dada wangu hawaja niita kwa jina lingine isipokuwa tu Filipo. Tangu kuzaliwa kwangu hadi leo, ninaitwa: Filipo! 

      Vema, jumapili iliyo pita mulijingojelea kusikia redio. Lakini ile mkutano haikufanyika! Hatunge kubali kukutana uso kwa uso ambayo ndani mwake wanaweza kutufilamu pasipo sisi pia kuwa na haki ya kufilamu. 

      Ninatamani,… Tutwae Mt.24:24… «Kwani kutasimama makristo wa uongo na manabii wa uongo ; na wataonyesha ishara kubwa na maajabu, kwa kudanganya, kama ingewezekana, hata wachaguliwa». Mufahamu haya: "Makristo wa uongo na manabii wa uongo..." ! Kwanza, mpakwa mafuta ni nani? Mpakwa mafuta ni mtu aliye na upako! Na upako huu unaweza kumuleta kuonyesha kila moja ya zawadi ya 1 Kor.12. Hakuna shairi la Biblia linalo tangaza mpakwa mafuta, wala si yeye anaye funguo za Ufalme wa mbinguni! Mpakwa mafuta ni mume au mwanamke anaye jitokeza akiwa na miujiza na maajabu pasipo Ujumbe! Miujiza ya mpakwa mafuta hayana mpaka ; anaweza kufufua wafu na tuliona katika Biblia Yane na Yambure waligeuza miti kavu kuwa nyoka. Kama Musa, walileta uhai kwa fimbo kavu! Lakini Musa alikuwa na Ujumbe. Sasa mutambue hii: kwanza, mpakwa mafuta anakuja na upako kama vile ilivyo maana ya jina lake. Hili ndilo jambo lake binafsi! Mpakwa mafuta maana yake: mtu anaye upako juu yake! Lakini kuhusu Neno, mpakwa mafuta hawezi kuja na ufunuo ya upekee ya Neno kwa kizazi moja kama vile tunavyo waona manabii wa Biblia lakini yeye anakuja na Neno lililo kuweko tangu zamani. Mpakwa mafuta anakuja na mambo mawili: "Imeandikwa" au "imeandikwa pia"! kwani hata salamu yake yaweza kuwa shairi la Biblia. Kama siyo: « Shalom » halafu ni: «Nakusalimu kwa maneno haya ya Paulo kwa Wakorinto! Nawasalimu kwa maandiko ya 2 Timotheo,… ».

      Lakini nabii anakuja pamoja na Neno kama ilivyo maana ya jina lake. Katika kiebrania, rabi maana yake: Mwalimu lakini neno nabii katika kiebrania ni Nabi maana yake: mjumbe toka uungu! Nabii anakuja na mambo nne: "Imeandikwa", "imeandikwa pia", "Ndivyo asema Bwana" na "Mimi, nawaambia"! Munaona ? Mpakwa mafuta anakuja pamoja na mashairi, na yote anayo yasema yanapashwa kuwa katika biblia lakini nabii analeta ufunuo wa siri zilizo fichwa ! Mpakwa mafuta hana hata haki ya kuondoa neno lililo andikwa. Inamubidi tu alitumie! Lakini nabii anaweza kusema: Mulisikia ikisemwa kwamba ni mto kule Edeni lakini mimi ninawaambia siyo mto wa kawaida lakini ni wa kiroho! Nabii anaweza kusema: Mulisikia kwamba malaika wawili walishuka kule Sodomo na Gomora lakini mimi ninawaambia kwamba hao malaika wawili siyo Gabrieli na Mikaeli wala Billy Graham na Osborn lakini ni Elia na Musa! Munaona? Nabii anakuja na ufunuo mpya, anatangaza hata maneno yasiyo andikwa! Kwa sababu yeye ni mwendelezo wa Biblia. Yeye ni mwendelezo wa ufunuo wa Mungu! Nabii anaweza kusema: mimi ni utimilifu wa unabii fulani ya Biblia, andiko hili la Biblia linasema tu kuhusu mimi peke! Nabii anaweza kusema: Musa alisema vile, lakini sasa, mimi, ninawaambia hivi! [Ndl:Kusanyiko linasema: "Amina!"]. Mtume Petro alisema: « Tubuni, na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo, kwa ondoleo la dhambi… » ! Lakini mimi ninawaambia: « Tubuni, na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo kwa urudishio »! Na ikiwa mimi ni nabii wa kweli halafu ubatizo yote ingine ni ya uwongo! Munaona? Ninaweza kusema: Muliambiwa kwamba kuna huduma tano lakini mimi ninawaambia kwamba kuna tu huduma nne za Neno! [Ndl:Kusanyiko linasema: "Amina!"]. William Branham na ukoo wake waliokolewa wakiwa na mabiblia King James, Scofield, Louis Segond,... lakini mimi ninawaambia kwamba King James, Scofield, Louis Segond ni pasipoti ya kwenda jehanamu! [Ndl:Kusanyiko linasema: "Amina!"].

      Mpakwa mafuta hahusike na ufunuo ya pekee inayo elekea Neno! Kwa uhakika anaweza kusema: "Mungu ananifunulia kwamba unaitwa hivi na kwamba utapata kazi, utapata mume,… Mungu ananifunulia kwamba utapata mtoto wa kiume tarehe fulani, ataitwa fulani!" Ni yote hii yeye anaweza kufanya. Na anaweza tu kuongoza watu, wala kwa Ukweli wala kwa uongo kwani mbali na nabii anayeongoza watu kwa Kristo, manabii na wapakwa mafuta wa dunia, wawe wa Mt.24:24 au hapana, wawe wa kweli au wa uongo, kazi yao tu ni kuongoza watu kwa… katika ono mapema, William Branham alipo uliza  wapi Bwana anapatikana, aliambiwa: atakuja kwanza kwako na itakuwa uamzi juu yako kulingana na Neno uliyo hubiri na kisha, utatuonyesha kwake! Utahukumiwa siyo kulingana na miujiza uliyofanya lakini kufwatana na Neno uliyo hubiri na kisha sisi wapakwa mafuta na waaminifu ambao tuliamini Ujumbe wako, utatuonyesha kwake! William Branham hakusema: Kama Paulo anaingia, sisi vilevile tutaingia kwani nilifanya miujiza kama yeye lakini alisema: Nilihubiri kama Paulo! Munaona? Wapakwa mafuta hawana nafasi yao pale! Katika nyakati za Noa, kila mpakwa mafuta wa kweli alipashwa kuongoza watu kwa safina ya Noa! Sababu gani? Kwa sababu Yne.6:28 ilikuwa ni Noa! Kazi ya Mungu, ilikuwa kumtambua Bwana wa milele, Mungu peke wa kweli na yule aliyetumwa naye maana yake Noa! Na Yne.3:16 ilikuwa: «Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtuma Noa nabii wake mpendwa ili kila mtu atakaye mwamini asiangamie katika garika! ». Munaona? Mpakwa mafuta anapashwa tu kuongoza watu kwa… Ni hivi tu! Osborn anapo hubiri katika nchi ya kigeni, anawaongoza wote wanao mwamini kwa kanisa lolote la kiinjili! Munaona? Tommy Osborn ni mpakwa mafuta wa Mt.24:24! Billy Graham ni mpakwa mafuta wa Mt.24:24! Moris Cerullo ni mpakwa mafuta wa Mt.24:24! Hata ukarimu mpya ya ukatholika ilipata wapakwa mafuta wakuu! Kama mtu hana ujumbe lakini anafanya miujiza, yeye siye nabii lakini yeye ni mpakwa mafuta! Haizuru ni roho gani inayo mtumia, haizuru anafanya nini, yeye ni mpakwa mafuta! Na kama pia mtu ana mwito, utume na ujumbe, yeye ni nabii! Joseph Smith ambaye aliweka misingi ya utaratibu ya wamormon ni nabii, Charles Russel ambaye aliweka misingi ya washuhuda wa Yehova ni nabii, hata Mohamad ni nabii ila tu wao ni wa uongo! Munaona? Kwa hali, wao ni manabii lakini kwa kilindi wao ni wa uongo!

      Mtambue tena jambo moja: nabii ni mpakwa mafuta lakini mpakwa mafuta siye nabii ! ninachukua mfano wa wapasha habari ! Mpasha habari ni mchangamuzi lakini karibuni wachangamuzi wote munao waona kwenye tv au kwenye redio siyo wapasha habari! Kati yao wapasha habari na wachangamuzi, wanajua lakini sisi tunao wasikiliza, hatujui! Munaona? Katika Afrika, tunapoona mtu aliye moja wa waganga au mtu anayevaa kanzu nyeupe, tunamwita daktari au mganga mkuu ijapo mtunzaji siye daktari! munaona?  Kuwa nabii ni kuwa na mwito, utume na ujumbe ambao siyo kurejea yaliyosemwa katika Biblia! Japo mpakwa mafuta anaweza kuja na huduma ya pekee ya uponyaji, mpakwa mafuta anaweza kusema kwa ufahamu maneno yote ya Biblia na kufanya miujiza kubwa na maajabu, Biblia inasema ya kwamba watazifanya, hata kufikia kuwadanganya wateule kama ingewezekana! Lakini mumutazame vizuri na mutaona kwamba hataweza kubatiza makanisa nzima. Anaweza kupatana, kuhusiana na makanisa, mitume na manabii, wainjilisti, waalimu na wachungaji hata pia kujulikana na kuonekana mkubwa kati kati yao lakini hawezi kuwabatiza tena. Lakini nabii mjumbe wa kweli hawezi wala kupatana wala kuhusiana na yeyote, hawezi hata kucheza na wa Barnaba wanao kataa kujinyenyekeza!

      Hao wapakwa mafuta na manabii wa Mt.24:24 wao basi ni huduma ya Ef.4:11! Kuna manabii wa kweli kama inavyo semwa katika Mdo.13:1. Wao ni wenye kuwa na ufunuo kamilifu zaidi na ya juu sana kuhusu maneno yaliyo semwa na nabii mjumbe lakini wanabaki tu katika mipaka ya maneno yaliyo semwa na nabii mjumbe! Kuna wapakwa mafuta wa kweli kama vile Filipo katika Mdo.8 kwa kupeleka ujumbe wa nabii mjumbe na wapakwa mafuta wa uwongo kwa kuwaongoza watu kwao wenyewe au kwa nabii aliye kufa imepita zaidi ya miaka 40! Kama Kumb.13:1 inavyo eleza, kila mara wanawaongoza watu kwa…

      Kwa kumaliza, mtambue tena kwamba kazi ya mpakwa mafuta inasimama katika mipaka ya inchi yake. Kwa mfano,  Zakpa Dadié ni mpakwa mafuta wa ubranhamisti! Kanisa lake lilipatikana tu huko Bouaké, pahali moja ambapo mashuhuiri Bara-Yesu [Ndl.: Kacou Sévérin] alianzisha huduma yake ya upako wa ajabu! Na huyu Zakpa alikuwa huko Bouaké vita ilipo anza tarehe 19 septemba 2002 na munakumbuka ginsi gani mji wake ulitekwa nyara na waasi na ginsi gani alitembea porini na mafundo miguuni kwa kuja Abidjan! Nilikuwa mwanzoni mwa huduma na hivyo hainge wezekana Abidjan ipatwe na hali moja na Bouaké kwa sababu niko hapa. [Ndl:Kusanyiko linasema: "Amina!"]. Na jumapili iliyo pita, japo ilinibidi nikutane naye, alikaa pale, macho yake yenye uzito, mlevi kwa pombe na watu wake walinuka pombe wakiwa na sigara mikononi, wengine kwa kapitula, wanawake katika suruali, mavazi yanayo pitisha mwanga pamoja na rangi juu ya kucha na juu ya midomo,… na yule mfugaji wa nguruwe aliweza kusema: « Nina waumini elfu nne katika miaka sita»! Alisema akiwa mlevi: «Nani alisema kwamba kunywa pombe ni dhambi? Muujiza ya kwanza ya Yesu ilikuwa nini? Ikiwa kuzini yapeleka jehanamu basi damu ya Yesu inafanya kazi gani? Msome Biblia vizuri, ni kukufuru Roho Mtakatifu ndiyo yapeleka jehanamu!... Branham ndiye nabii wa mwisho… »! Munaona? Watu kama hawa kama munawaona wakifa na njaa na munatupa mabaki ya chakula chenu kwenyi tupio la uchafu, hamufanyi dhambi kwani, Mungu anapo sema: utampenda jirani yako kama ujipendavyo, hakutaja shetani! [Ndl:Kusanyiko linasema: "Amina!"]. Ndugu na dada, nyoka na nguruwe siyo jirani wenu! Munaona ? Kama Adamu na Eva wangeelewa, mambo hayange kuwa hivi katika Edeni! Munaona ? Jirani wako, ni yule anaye sema: « ninatamani kwenda kanisani lakini nimeelemewa na sigara au pombe»! Jirani wako ni yule mdogo anaye sema: « Ninatamani kwenda kanisani lakini maisha yangu hayalingane na ya mkristo, mimi ni mchafu sana»!

      Japo watu hawa wanaweza kuwapeleka kwa maungamo hazarani pasipo nyinyi kujua! Kama mababu zao katika Edeni, wao ni wasujaa katika dhambi! Wanaweza kuwaomba soda na hapo munapo waacha, wanarudi dukani kwa kuibadilisha na bia! [Ndl:Kusanyiko linasema: "Amina!"].

       Nitasoma sehemu moja katika kitabu cha majani kwa kumaliza. Ni katika ukurasa 120… « Mnapashwa kujua kwamba wakati ya kuzini, nyoka alikuwa na umbo lake la kibinadamu. Basi, huyu mtambazi aliye porini ni baba ya Kaina kama vile nilivyo baba wa Neema. Mfupa kwa mfupa, mwili kwa mwili. Huyu mtambazi munaye muona porini ni babu ya wote wanao hukumiwa na Ujumbe huu na ambao hawawezi kutubu. Nina leta upingamizi kwa waganga waweze kupima ADN ya damu yao na waniambie ni uwongo gani ninasema! Nilisema kwamba nyoka anapo uawa, wanamemba wa haya makanisa za kikatolika, protestanti, kiinjili na kibranhamisti walipashwa kuiheshimu. Munaona kwamba katika Afrika makabila mengi hawale nyama moja moja kwani waliambiwa kwamba zamani, babu wao kwa ajili ya jambo fulani, alijigeuza au aligeuzwa kuwa mnyama huu na ni kweli… yeye ni mnyama lakini yeye ni babu wa kabila moja la watu. Kama alizaa watoto kabla ya kugeuka mnyama, yeye anadumu kuwa baba wa watoto wake ! Haya ndiyo mambo yaliyo pitika katika bustani la Edeni. Na leo, ni alisi kwa mubranhamisti kuinamisha kichwa juu ya maiti ya nguma… » ! Angalieni ginsi gani nyoka walisimamiana pale kaburini kwa mazishi ya Kacou Sévérin, wanapo weka uwasiwasi kaburini kule! Ilikuwa uthibitisho wa Kelele ya Usiku wa manane ! Na mke wa Kacou Sévérin alisema katika gazeti moja kwamba ilikuwa nyoka ya kawaida kama kila nyoka ! Hakika ! Ni nyoka ya kawaida kama kila nyoka lakini ni babu wa Kacou Sévérin na wa wapakwa mafuta wote na manabii wakatholika, waprotestanti, wa kiinjili na wabranhamisti!


Tuma ukurasa huu kwa rafiki

kurudi kwa utaratibu

www.matth25v6.org - Copyright © Aprili 2007
Kisheria Deposit ® All rights reserved