MAHUBIRI N°8

MKUTANO WA KIEKUMENIKA

(Ililetwa januari 2003 pa Locodjro, Abidjan – Côte d’Ivoire)



      Manabii waliinenea, na sasa imefika siku hii ya nne tarehe 09 januari 2003. Alama ya historia imeletwa. Biblia na korani zimekutana. Wakatolika, waprotestanti, wa kiinjili, waislamu, wabudha, wamahikari, warosikrusia, dini za asili, eckankar, imani baha’ie, wakisiasa, orodha za kisiri… wamekutana nyumbani mwa michezo ya Treichville kwa kuomba. Kuomba nani? Sijui! ni juu zaidi ya mawazo yangu. Ni juu zaidi ya CNEPE-CI na ya shauri la makanisa ulimwenguni. Ni ile ambayo mwanadamu hakuweza kufikiria. Na, kwa mfano ya wote waliyo nitangulia katika nyakati za kale, nilikuwa pale! Nilifikiria kupata pale manabii, hawakuwa pale. Ni wapi watu wa ukweli kwa hiyo miadi la historia? Niliona baragumu na umeme ya hasira juu ya nyumba la michezo. Kisha, niliona patwa jua  (mwezi). 

     Kesho baadae, niliona juu ya gazeti ya kiinjili, kichwa hiki cha makufuru: « Biblia inajiunga kwa Korani » ; kardinali Bernard Agré, mwalimu Idriss Koudouss, rev. Ediemou Jacob aliye mpotevu mkuu wa wachawi wa Côte d'Ivoire, rev. Benjamin Boni, presidenti wa kanisa méthodisti iliyo ungana… mkono mkononi. Sikusema siku zote kwamba shetani ndiye mungu wa makanisa zote hizo, na popo ni mfano wao wa kiroho? Mungu hakuweka popo katikati ya mtaa ulio katikati ya Abidjan, moyo wa Côte d'Ivoire? Mapema basi tarehe 09 januari, nilikuwa pale, na polisi na waaskari wa gereza na tayari, Biblia ikinyanyuliwa juu ya nyumba, nili paza sauti bila kuchoka kwa megafone: "Ni asubuhi hii maadui za Mungu watakusanyika nafasi hii! ni asubuhi hii ndipo maadui za Mungu na za nchi watakusanyika hapa!" watu walinisihi niseme: " marafiki na maadui za Mungu…" na walipoona kwamba hawawezi kunishawishi, wakachochea polisi na waaskari wakisema: "musemwa wake unatusumbua, hatuta weza kuomba ikiwa mgongoni! Mumufunge!" sikuwasikia. Karibia saa tatu ya asubuhi, mkuu wa polisi alitoka nyumbani ili aje anitie kifungoni alipo sukumwa lakini sikuacha. Tulijibiana ndipo akafahamu. Na tena polisi wengine wawili wakaja lakini sikujiona kuachilia kabla saa nne ya mchana itimie. Na ilikuwa hivyo hata saa 4:30 ya mchana.  Na pale, mtu mmoja aliye vaa koti akajionyesha kwangu kwamba yeye ndiye katibu ya taifa wa CNEPE-CI alitoka nyumbani pamoja na mwingine aliye vaa kanzu nyeusi. Alisikia wakisema juu ya Kacou Filipo lakini hakujua kwamba ilikuwa ni mimi. Alisema: "Tangu asubuhi unakuwa ukirejea tu ile musemwa. Rais wa jamuhuri na wakuu watakuwa hapa na ile haita onekana vizuri." Tena akaomba polisi wanifunge. Mkuu wao akawaambia watu wake: "akarejea, mumufunge". Nilisema:" kama ninapenda kuendelea nitaifanya kwani Biblia haiwezi kutii kiyungulo ! je! ni wewe uliyo nituma kuwa hapa?" alisema: "Umekuwa kwa mpaka wetu!" nilisema: "mimi ni mkristo, ndio maana niko hapa!" Nilizungukwa na polisi wakiwa tayari kunifunga lakini nilisema kwa ukali hata akabadilisha: "musimutie kifungoni lakini mumunyanganye megafone!".

       Na asubuhi ile, dini zote zilikuwa pale, kwa mustari moja: waislamu wakivaa kanzu, wakatoliki, wa Eckankar,… na walinitazama wote kama watu ambao hawakuji kwa kusali. Walinitazama kama mimi ndiye shetani wao ijapokuwa walikuja kwa kuomba…

       Neno la katibu wa CNEPE-CI ilikuwa kama upitishiaji wa mapepo kwa askari polisi kwani walichochelewa. Kulikuwa na askari, polisi wa gereza na askari polisi na kulikuwa na mubranhamisti, baba wa ndugu moja hapa kati ya waaskari… Ijapo, niliona andiko la makanisa zote juu ya mlango wa nyumba. Ukiwa mwanamemba wa kanisa moja, yenyewe kiungo cha CNEPE-CI alafu wewe ni mwenye makosa mbele ya Mungu hata ikiwa haukuwa kwenye uwanja. Makanisa walipokea msaada kwa mapepo ile tarehe 09 januari na ni kwa ajili ya uamsho wa watakatifu iliyo sasa duniani kwa huduma hii ya Mat.25:6. Na tayari  kwa wamoja-wamoja kati yetu kuna ile nguvu, itakayo anzisha ule uamsho. Na niliwaambia kwa neno la Bwana kwamba uamsho itasukumwa na CNEPE-CI, hiyo onyesho la shetani ambalo si jambo lingine ila sanduku la wachawi waliyo vikwa ngozi ya kondoo. Mukitambua, mkuu wa CNEPE-CI na mtu aliyevaa kanzu nyeusi walitoka nyumbani, kaburini pamoja na garika la mapepo ambao alipitishia polisi. Mutazame Mat.8:28-34, Yesu alipo mponya huyo mtu mwenye pepo wachafu huko Gerase, wale wale mapepo wakaingia ndani ya nguruwe kisha ndani ya maji… kisha ndani ya wachungaji,… kisha ndani ya wakaaji wa kijiji na hao wakafukuza Yesu.

     Tangu nyakati za kale, wote ambao Mungu alipandisha walifanya hivyo hata bila mali, kwani kazi ya Mungu haihitaji pesa pia, kubaki hekaluni kwa ku hukumu siyo kazi ya Mungu lakini ingine sura ya udanganyifu. Siyo hiyo manabii, mitume na Yesu mwenyewe walitufundisha kwa huduma yao. Kweli inashinda na inajiweka kwa nafasi, hapana ndani ya makanisa wala ndani ya makesha ya maombi. Ikiwa hauna pesa, endelea! Nilihubiri popote mpaka sasa bila kupokea kitu kwa mtu isipo kuwa tu mtu aliye niletea mchele nyumbani. Ijapo, sikuona mwinjilisti au nabii ambaye hakupokea hundi za benki, nyumba kubwa kubwa, gari na viengine. Usitamani ambacho hauna. Kwa injili hiyo, nimechagua njia nyembamba pamoja nanyi basi tusimame imara! ikiwa mbingu imefichwa kwao siyo mali yao itakayo pata njia. Ikiwa haikupewa kwako toka mbinguni kabla kuwekwa msingi dunia, hauwezi kumupa mchaguliwa hicho kikombe cha maji cha Mat.25: 32-35. Kile walitendea mti mbichi ndicho watatendea mti ya kukauka. Mtumishi si mkuu kuliko bwana. Munaona? Hii tarehe 09 januari, nilipo paza sauti toka saa moja mpaka saa nne ya mchana, nilitamani baki la maji ambalo walikuwa wakitupa lakini ikiwa mtu angejaribu kunipatia, makutano wange mugeukia. Munaona? Walinitazama kama watu ambao hawakuji kwa kuomba. Macho ya Kaina! Kulikuwa na waislamu wanaovaa kanzu, wametodisti, wakatolika, wabatisti nilio wajua kwa sura, shemeki yangu, mume wa binti wa mjomba, aliye muhubiri mumetodisti alikuwa pale… Munaona? Mbuzi, kuku, mbwa wote pamoja.

     Hubirieni! Musiogope wanao jidai kwamba wao ni manabii. Ni zile roho za uchawi tu ambazo zimejiweka ndani ya makanisa. Biblia iliitabiri katika Mat.24:24. Nabii gani? Kwa huduma zote, [maisha] ya kale ya nabii yanahesabiwa. Tangu kuzaliwa kwake. Hata mchungaji! Mtu aliye na mtoto nje au kabla ya ndoa hawezi kuwa mchungaji. Anaweza kufanya kazi ya mchungaji lakini hawezi kuwa mchungaji. Muinjilisti, ndiyo; lakini hapana mchungaji au nabii. Ni sawa sawa kama mke wake si mtiifu au ikiwa ana mtoto nje ya ndoa. Angalieni Yeremia 1:5, Waamuzi 13:3-4, Luka 1:13-15,… haifai uwe mtu aliye ishi maisha mabaya wakati uliyo pita, kujuwa wanawake, kukunywa pombe ya kulevia, au kuvuta sigara na baadae kugeuka mchungaji au nabii wa Mungu; haizuru maono unayo. Anaweza kufanya kazi ya mchungaji kwa muda lakini yeye si mchungaji. Ni hivi. Kwa nabii au mchungaji, inabidi ushuhuda… inakubidi utimize mapashwa kama sivyo, baki mtulivu!

     Sizarau pia sheria na manabii wanao sema kwamba atakuwa na mke moja ambaye bado hajaguswa [Law.21:13-14 / Ezekieli 44:22]. Mke wangu alikuwa na miaka hishirini kwa mwaka 2000 nilipo mwoa na sikujua kwamba alikuwa bikira. Na hiyo kwa wakati ambapo ni magumu kupata bikira kwa umri wa miaka kumi na tano. Na ikiwa mume alijua bikira kabla ya kutoa mali juu yake, hawezi kuhesabiwa kwamba alioa bikira.

     Ambacho hukupewa na Mungu toka mbinguni, usikitamani. Kumbukeni kwamba mbinguni, malaika wote waliotamani kuwa na huduma kubwa kama ile ya Gabrieli wakatupwa duniani. Ikiwa Mungu alikutuma duniani kwa ajili ya kazi fulani, atakuchunga katikati ya hii viozo. Huduma siyo jambo la kuhubiri vizuri au kupaza sauti na kuruka ruka mbele ya watu…

Basi, Mungu akapiga kwa upofu mji iliyo kuwa yenye kumuasi. Lakini katika huruma yake, akawatumia mtu kwa kuwaponya. Lakini wakasema: "Hatutaki tena kuona kwani tangu tulipofushwa, tuna yote kwa bure, na dunia nzima inatushughulikia. Utuombee basi msamaha kwa Mungu na ni nini inaonyesha kwamba ni Mungu aliye kutuma?" siku moja, kijiji jirani ika jiuliza na kusema: "tunalima, tunateswa na udongo haitupatie tena mavuno. Tunafariki ijapokuwa kijiji mpofu ina yote kwa uwingi. Twendeni, tuwaue na tukamate udongo yao na yote waliyopewa. " wakatwaa fimbo kubwa kubwa mchana kati, wakakwenda katikati ya kijii mpofu na wakaanza kupaza sauti: "Muje kwetu! Tumekuja na mifuko za mchele, mafuta, nguo,… sisi ni shauri na shirikisho la makanisa, sisi ni ndugu zenu katika Kristo". Wakatoka lakini nabii alipo waona akajiokoa na jamaa yake. Na jirani wao katika nyara wakatoka na wakaanza kuwaua… wamoja walilalamika: "Muturehemu! Ô Rehema!" na walikimbia mikono ikinyoshwa mbele namna hii! Wengine walilalamika: "lakini iko nini?? muwashike!! Muwashike!! ". Wandugu, ilikuwa huruma. Kijiji ikakoma. Tena katika uchungu wao, walilia wote: "Tunatamani kuona, tunahitaji huyo nabii, tunatamani kuona tena…". Wale ambao hawakutoka wakauawa pia, wakapokea chapa.

      Kama ilivyo kuwa wakati wa Noa, vivyo hivyo itakuwa kwa kizazi hiki kikaidi na makanisa zake. Aliye na masikio ya kusikia asikie.


Tuma ukurasa huu kwa rafiki

kurudi kwa utaratibu

www.matth25v6.org - Copyright © Aprili 2007
Kisheria Deposit ® All rights reserved