Tangu 2002, nilipoanza kuhubiri ufunuo juu ya Biblia, wachungaji na manabii wajanja walipo kutana na ujumbe, walianza kulazimisha Biblia Darby katika makanisa zao badala ya kuja kukubali ujumbe. Ijapo, wanaweza kubadilisha biblia lakini hawataweza kubadilisha iliyo ya muhimu ambayo ni roho ya uchawi itakayo wapeleka kuzimu. Munaona? Na tangu hii mwaka 2003, ma mia za ukurasa zimetumwa duniani juu ya internet. Na tunaona mara kwa mara wachungaji, manabii, wainjilisti wakiwa na Darby. Wameweka vyombo kubwa kubwa vyao vya uchawi ambavyo ni Louis Segond, Scofield, Thompson, King James,...kwa hivyo ninaamini kwamba, mapepo za uchawi tunazo zifukuza kutoka hapa zinaweza kwenda kuwafunulia mambo yale kwa kufuruga pahali imetoka. Wamoja wanaona kwamba ni kweli lakini kwa kukubali, watapoteza nini?... Mukumbuke Matayo 8:28-34, Yesu aliokoa wababa wawili wa jamaa waliyo rudi nyumbani mwao. Ingebidi iwe karamu kwa utukufu wa Yesu, lakini watu walipoona kwamba iliwaleta kupoteza zizi la nguruwe, hawakufurahi, wakafukuza Yesu.…
Vema, kuna wingi wa ukweli lakini moja tu ni Kweli, kuna miungu nyingi lakini moja tu ni Mungu wa kweli. Kuna makanisa nyingi lakini kuna moja tu iliyo Kanisa la kweli. Kuna maroho takatifu nyingi lakini kuna moja tu iliyo Roho Mtakatifu wa kweli. Kuna tafsiri nyingi za Biblia lakini moja tu ni tafsiri ya kweli.
Juweni kwamba kwa nukta hiyo ya ujumbe, mabishano mengi yametupwa duniani. Nitaambiwa: "Halafu wale wasiyo na tafsiri Darby katika lugha yao?" Musiogope! Sitaki kuwaondolea Biblia. Sijui namna gani lakini tafsiri Darby itatafsiriwa katika lugha nyigine. Kwa muda wa miaka 1500, baba zenu hawakuwa na Biblia lakini waliishi ukristiani vizuri sana kuliko ninyi. Wanao tangaza tafsiri Darby, badala ya kutafuta kuitafsiri kwa lugha nyingine, wanatafuta namna ya kuirekebisha. Wote waliyo sahihi ma tafsiri katika historia walikuwa wahubiri wakuu, waliyojazwa Roho. Siyo kundi la wenye elimu… Kiebrania ya kale haisemeki tena na ni lugha ngumu kuliko lugha zote zinazoweza kupatikana, pasipo herufi za sauti, lakini ni rahisi kutafsiri kutoka Darby hata lugha nyingine kama pia siku moja, ujumbe huu utatafsiriwa katika lugha nyingine nisizoweza kufahamu! Munaona? Ni ile iliwabidi wafanye. Kwa yote, siaminie marekebisho hata moja. Kuendelea kwa lugha inabidi maandiko ya kufasiria chini ya ukurasa, hapana marekebisho. Kila mara Lugha zitaendelea. Sasa, kufwatana na neema niliyo pewa, naona kwamba sasa, Tangu huduma hii ya Mat.25:6 na Ufu.12:14, kuwa na tafsiri ya biblia ambayo Roho inahukumu ni tendo la maasi. Na pia kuwa na tafsiri Darby niliyo amuru na kubaki mbali na ile Mungu iko akifanya haibadilishe kitu. Kuna wokovu tu katika kile Mungu iko akifanya.
Vema! Katika Isaya 35: 8-9: ni njia iliyo takatifu, siyo njia kubwa. Katika Waamzi 17:1-5, ni mungu (sanamu), wala siyo Mungu. Someni mpaka Waamzi 18:23-24 pahali Louis Segond anatambua kwamba ndama ya zahabu ni mungu na katika 1Fal.12:28, anaandika “Mungu” kwa ndama za zahabu.
Katika Ezekieli 2:1; 3:1, 4:1,... ni "mwana wa watu " maana yake nabii wala siyo "mwana wa mtu " inayo semwa kwa Yesu-Kristo, nabii mkuu sana kama katika Mat.16:13. Ndiyo maana, katika Ezekieli 3:12 na 14 kama katika Ufu. 14:13, ni Roho ya Mungu ni kusema “R” kubwa kama katika Ez.8:3.
Katika Mwa.1:2 ; 1Sam.16: 4 ; Isaya 61:1,... "R" inabidi iwe herufi kubwa wakati ni Mungu. Lakini, sababu ya kweli inayo mtuma Louis Segond aandike “[r]oho” ya Mungu na “r” ni kwamba, kwa mafikiri yake, kuna roho nzuri ya Mungu na roho mbaya ya Mungu. Siamini mafundisho haya. Na hiyo inafunuliwa katika 1Samueli 18:10. Louis Segond anasema: "… roho mbaya ya Mungu ikashika Saulo..." ijapokuwa Darby anasema: "...roho mbaya moja iliyo tumwa na Mungu ikashika Saulo." Ni namna moja kwa 1Sam.19:9.
Katika Mat.24:24, "K" ya makristo ya uongo inabidi iwe kwa herufi ndogo kwani siyo Roho Mtakatifu wa kweli lakini roho za uchawi ambazo zilibidi kutenda kama roho mtakatifu. Hivyo “makristo wa uongo” wala siyo ma Kristo wa uongo”.
Katika Ufu.1:4, ni “Roho” kwani ni Roho Mtakatifu katika mipango saba.
Onyesho la “mwana mzaliwa wa kwanza” katika Mat.1:25 kwa kusema kwamba Maria hakuwa na watoto wengine nyuma ya Yesu. Ni kwa kusudi walifanya mambo yote hayo kwa shabaha za kidini.
Herufi ndogo ya kristo au bwana Yesu hasa ndani ya Agano Jipya,… zinajibu kwa Lugha ya kiyunani ambayo inaruhusu herufi kubwa tu wakati neno inakamata maana ya jina la upekee.
Mat.4:10,… Kuabudu ni tafsiri neno kwa neno ya neno ya kiyunani proskïneo.
Katika Ufu.1:20, ni taa saba za zahabu (kinara moja) wala siyo vinara saba vinavyo leta taa makumi mane na tisa; sawasawa katika Ufu.11:4.
Katika Yoane 17:11: "ninakuja kwako” wala siyo "ninakwenda kwako” kwani Baba ni ndani mwake; pia kwa shairi la 12, ni: “jina lako ulilo nipa”.
Katika Danieli 5:25, Louis Segond hakutia andiko lililo chapwa juu ya ukuta: "Mene, Mene, Tekeli, Ufarsini!". Juweni hapo kwamba Ufarsini ni uwingi ya Peresi.
Katika Danieli 9:25-27, kuna mchanganyiko katika tafsiri juu ya “juma 70 za Danieli” kama Mika 1:10-15 ambayo Louis Segond alipata magumu kwa kuitafsiri. Darby anasema katika Mika 1:10:"… katika Beti-Leafura, ujiviringishe mavumbini ". Louis Segond anasema: "…ninajiviringisha mavumbini katika Beti-Leafura ". Munaona?
Katika Mat.24:28, ni “tai”. Ni pahali pia ya kukamilisha kwamba yaliyomo katika tafsiri za Louis Segond ni mbalimbali... mutafsiri asingeweza kufahamu lugha zote za dunia, mtu aliye na Roho angelipaswa kutafsiri kwa mfano toka Darby hata Portugal, kihispania,… kwani ya muhimu ni kwamba ifanyike katika lugha ya mjumbe na kwa neema ya Mungu, ni namna hiyo.
Katika Ufu.1:10, ni “mchana” (jumapili) wala siyo “siku” ambayo inaweza kusemeka kwa siku ya unabii ambayo ni miaka elfu.
Katika Mwanzo 4:15, ni atakaye muua Kaina ndiye atahazibiwa mara saba wala siyo Kaini atakaye lipishiwa kisasi mara saba. Darby anasema: «Na Bwana akamwambia: ndio maana yeyote atakaye muua Kaina atahazibiwa mara saba… » Louis Segond anasema: “Bwana akamwambia: kama mtu akiua Kaina, Kaina atalipizwa kisasi mara saba…". Siyo namna moja. Na katika Mwanzo 4:23, 24, mteolojia Lemeki aliitafsiri kwa nia yake kwa kumwanga damu kama babu ya babu wake ambaye ni Kaina.
Mat.11:23: "hadese*" si lazima iwe "kuzimu" kwani kuna kwa upande moja hadese* iliyo pahali pa masumbuko na kwa upande mwingine kifua cha Abrahamu.
Katika Ebr.13:17, Louis Segond anasena: «Mutiini viongozi vyenu na muwe na unyenyekevu kwao, kwani wanakesha juu ya nafsi zenu… ». Lakini Biblia inasema kwamba kuna moja tu anaye kesha JUU ya nafsi zetu na pia JUU ya nafsi za viongozi vyetu, ni Mungu.
1 Kor.11:15 inamalizika na nukta (wala siyo alama ya swali) kwa kumalizia kwamba nywele ndefu ni kitambaa cha mwanamke. Ma kamati walio rekebisha Louis Segond walitambua hiyo. Katika Rom.16:1, siyo “shemashi” lakini “mtumishi”. Shairi la 2 inaionyesha. Alikuwa msaada kwa watakatifu, ni hiyo alifanya.
Ufu.12:18 ni sehemu ya kifungo cha kwanza cha sura ya 13 na pia siyo: “akasimama” lakini “nikasimama…” kwani siyo joka lakini Yoane.
Ile kazi moja juu ya Louis Segond ilifanyika pia kwa ma tafsiri King James, Ostervald, David Martin,... kwa sababu kila moja ya zile tafsiri inatawala kwa pahali Fulani ya dunia. Kuna nchi pahali Louis Segond hajulikane. Shetani amefanya kazi ya kilindi na watu hawajui. Munaona? Tena, Louis Segond amefanyizwa marekebisho mengi, jambo ambalo halikufanyika bado kwa Darby. Ijapo tunajuwa ya kwamba ni kwa sababu jambo Fulani ni mbaya ndipo linarekebishwa. Hivyo, kamati za marekebisho hazikuheshimu aya zilizo katika zile za asili ya kiebrania na kiyunani. Na wingi wa mashairi ziliongezwa kwa ajili ya maelewano.
Nina ripoti kwamba tafsiri za Scofield na Thompson zinatoka katika zingine, zilitoka katika Louis Segond. Kwa jambo linalo husu King Jams (mfalme Yakobo), mufalme Jacques IV wa Scotland alipo kamata kiti cha ufalme cha Uingereza na jina ya Jaques 1er, akaomba kwa watafsiri makumi tano na nne wakuu sana wa London, wapagani kama wa kidini, wafanye tafsiri inayo itwa kwa jina lake, namna moja ya kupata neema ya wakristo. Ni kama wangelipatia dunia nzima tafsiri nzuri sana inayoitwa: Tafsiri Fidel Castro au hata Tafsiri mfalme Bokassa 1er.
Lakini, kitu cha kwanza cha mapingano ni: "Louis Segond, mwalimu katika teolojia" kwa ukurasa wa kwanza wa ile biblia. Kukubali hiyo, ni kukubali teolojia kwani ninapo jua kwamba uchawi siyo nzuri, namna gani naweza kusoma biblia iliyo tafsiriwa na mchawi na inayo kwa ukurasa wa kwanza: "Tafsiri ya Zérédji, mchawi mkuu" hata ikiwa imefanyika vizuri? Kwanza pale, nina sifu waprotestanti na wakiinjili kwani, wanapo hukumu wakatolika, hawatumii biblia Tob. Wakiinjili na wateolojia watasimama siku ya hukumu kwa kuhukumu wabranhamisti. Munaona? Wabranhamisti wanapenda kuonyesha wanadamu kwamba mti mbaya wa teolojia ambao Branham alihukumu unaweza kutoa matunda mema. Na watajibu kwa hayo mbele ya Mungu.
Ikiwa mwanamemba moja wa kanisa la kiinjili hajui sababu gani hizi mabiblia Louis Segond, King James na zingine ni za shetani, nawaomba mumufasirie vizuri sana kutoka teolojia hata kufikia ulinganisho wa mashairi. Lakini ikiwa wabranhamisti, wana wa Beliali wanapinga hii ujumbe, inatokana na nia mbaya au kiburi kama sivyo ni walozi kwani hawawezi kusema kwamba hawafahamu…
Kuhusu kugawanywa ya Biblia kwa sura na kwa mashairi, kwanza kwa karne ya IX, waliyo na elimu ya kutumika juu ya Biblia (wakuu wa dini na waakili wa kiyahudi) wakaingiza hesabu katika kiasi cha maandiko ya Agano la Kale wakiacha aya namna zilizo, bila kuzibadilisha. Tena kwa karne ya XIII, watu wawili: kardinali moja muhispania aliye itwa kwa jina la Hugo na askofu mkuu muingereza aliye itwa kwa jina la Langton waka gawanya matafsiri za kwanza kwa sura. Ni kwa mwaka 1520 ndipo Sanctès Pagnin alitia hesabu katika kiasi cha tafsiri yake ya kilatini sawasawa na maandiko ya kiebrania kwa mfano ya tafsiri Darby, bila kutofautisha mistari. Lakini kwa mwaka 1551, Robert Estienne, katika tafsiri yake ya kiingereza ya Agano Jipya iliyo tokea Geneva, aliifanya kama Louis Segond, akigawanya maandiko kwa mashairi na kila shairi kwa mistari, hivyo akaharibu zile aya za vitabu vya kiebrania na kiyunani. Robert Estienne aliifanya kwa kutangaza vulgate yake iliyotokea kwa mwaka 1555. Njia hiyo ya kishetani ikakubaliwa kwanza na kundi la makuhani wa Ufaransa na vyama vikuu vya kiinjili vya wakati ule. Ni hivi sasa kwa Darby, tunajua kwamba Ufu.12:18 ni shairi la kwanza la Ufu.13. « [Ufu.12:18:] Na nikasimama juu ya mchanga wa bahari; [Ufu.13:1:] na nikaona nyama akitoka katika bahari mwenye pembe kumi na vichwa saba, na juu ya pembe zake taji kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru». Na ndani ya Darby, asterisk zinaonyesha mwanzo wa sura za [maandiko] ya asili ya kiebrania. Kwa hivyo, Mwanzo 2:4 ni mwanzo wa sura 2 ya Mwanzo na ni vile katika Biblia yote. Munaona kwamba Mwa.2:1 inasema: “Ndivyo zikamalizwa…”. Munaona kwamba ni mwanzo ya kumalizia sura ya 1…
Kufwatana na historia, John Nelson Darby alizaliwa London kwa mwaka 1800 na baba wa Irland. Yeye ni wa asili ya Irland kama William Branham. Nyuma ya masomo yake mengi ya haki kwa chuo kikuu cha Dublin (Irland), akatoka akiwa mwanasheria kabla ya kuacha kundi la wanasheria kwa kumfuata Bwana. Kama Wesley kwa mwaka 1725, akawa shemashi mdogo wa kanisa la anglikani kwa mwaka 1825 baada ya hayo [akawa] mchungaji mwaka iliyo fwata katika mji wa Wicklow huko Irland kabla ya kuachana na kazi hiyo baada ya kukosa masikilizano na wakuu wake [wa kazi]. Baada ya masomo mengi ya mwanasheria, kitu moja ambacho Darby alijifunza ni lugha [nyingi] ijapokuwa alizungumza kiebrania na kiyunani kama lugha ya kale yake ya kuzaliwa. Kujifunza lugha siyo teolojia! Kwa kufwata, rafiki wake J.G. Bellet, yeye pia mwanasheria, akamfwata. Tangu pale, akitegemea tu Roho Mtakatifu, Darby akaanza kuhubiri katika vijiji na kampeni tangu Irland, kupitia Ulaya, Asia na Amerika akihukumu shirika la kanisa, urais wa kanisa kwa mtu, anasa, teolojia na akionyesha hapo kwamba “Yesu Kristo ndiye Yehova wa Agano la Kale”, akialika makanisa zote kurudilia msingi ya mitume na ya manabii. Darby alizungumza kiingereza, kifaransa, kiebrania, kiyunani, kijerumani, na kiitaliano. Alitafsiri Agano Jipya na la Kale kuelekea mwaka 1859 kabla ya ile ambayo Louis Segond alitafsiri kwa ombi la kampuni la wachungaji wa Geneva. Kwa hivyo Tafsiri Darby ikapita ile ya King Jams ambayo mfalme Yakobo aliomba waifanye kwa jina lake, na iliyo fanyika kwa mwaka 1611, tafsiri ambayo ilitawala kwa muda wa karne mbili na ilikuwa ni kurejea katika ile ya William Tyndall. Mufalme Yakobo mwenyewe alikubali waakili 47, watafsiri wakuu kwa hesabu yao inabidi kuongeza hesabu Fulani ya wakuu wa dini wayahudi waliyo kuwa na maandiko mazuri sana ya mikono na wote waligawanywa kwa kundi kubwa tatu. Kundi moja kwa chuo kikuu cha Cambridge, kundi lingine kwa Oxford, na kundi la mwisho huko Westminster. Na kila kundi liligawanywa pia kwa kundi ndogo mbili. Kwa jumla ni kundi sita. Kundi la kwanza lilipo maliza lilipitisha kazi kwa kundi la pili ambalo pia lilipitisha kwa [kundi] ifwatayo…lakini japo hivyo, kulikuwa kusahihisha mara kumi na nne kabla ya onyesho la kwanza la King Jams kwa mwaka 1611. Ijapo kila moja wao alijuwa sana kiebrania kuliko haizuru muyahudi Fulani. Na ilisemwa kwa moja wa watafsiri wa ile biblia King Jams kwamba alikuwa msujaa sana katika lugha zote, hasa zile za mashariki, kwamba angeli kuwepo kwa mchanganyo wa lugha kwa wakati wa mnara wa Babeli, angeliweza kuwa msaada kama mtafsiri. Munaona? Na babu ya babu ya mtu kama huyu alikuwa mjengaji wa mnara wa Babeli na tazama mjukuu wa mjukuu wake ni mjengaji wa mnara wa Babeli mpya uitwao “biblia King Jams” katika hiyo Edeni ya Shetani. Lakini riziki ya Mungu ikafanya kwamba Darby, mtu moja tu, akasimama kutoka kwa Mungu kwa kutafsiri Biblia. Je! Mungu mwenye uwezo ana haja ya waakili makumi tano na nne kwa kutafsiri Biblia? Je! Mungu hutumika pamoja na wenye akili?...
Tafsiri Darby ikapita pia ile ya mteolojia mkuu Ostervald iliyo toka katika marekebisho ya mwanaelimu na mteolojia David Martin [kwa ombi la mkutano wa makanisa za Wallonnie] juu ya biblia ya Lemaistre de Sacy. [Kumbuka: nili gundua kwa juni 2005, kwamba John Nelson Darby alikwenda mbali sana katika tafsiri ya siri za Biblia, akionyesha tayari kwa karne ya 19 kwamba wazee 24 kando ya kiti cha enzi ilikuwa wote pamoja mitume 12 na baba 12, kwamba Mwa.1:27 siyo kwa ajili ya malaika,…].
Biblia moja tu iliyo shinda na ambayo bado haikuguswa upya wala kurekebishwa hata na Darby mwenyewe na ambayo haikuwa rejeo au tafsiri kutoka tafsiri ingine ni tafsiri ya mwanasheria John Nelson Darby. Na ningependa tafsiri ya kifaransa itumiwe kama msingi kwa tafsiri katika lugha nyingine pamoja na daraja (au mafasirio) juu ya maneno zilizo zeeka. Na nilipata ufunuo kwamba ni Biblia ya Bibi Arusi kabla ya kupata hizo habari. Darby alikufa tarehe 29 Aprili 1882 na tazama maneno yake ya mwisho: “Mungu abarikiwe, sizani kuwa na la kuondoa, wala kitu kidogo ya kuongeza. Sina la kuongeza isipo kuwa shukurani na upendo wangu kwa kweli kwake” (Barua ya 19 Machi 1882). Maneno haya yawe pia yangu kwa mwisho wa ujumbe huu na nipewe sawasawa kwenu mulio amini, sifa za ushindi na ni juu ya ile tunategemea! [Kusanyiko linapaza sauti: « Amina !»]. Nimesema niliyo ona na yale Mungu aliyo niamuru kusema kama kwa Musa, Paulo… niliitwa kwa namna isiyo ya kawaida na nilitumika kama wao, kama wakiingia, sisi pia tutaingia [kusanyiko linasema: Amina!]. Ni yasiyo weza kuanguka!
Maandiko matatu ya mkono yanayo julikana sana ambayo yanakusanya karibu canon yote, vitabu vya agano Jipya nzima na la Kale ndivyo: Sinaïticus iliyo gunduliwa kwa karne ya 4 katika utawa mtakatifu Katherine ya mlima Sinai. Ina Agano Jipya na la Kale nzima; kwa leo imechungwa katika British Museum ya London. Kisha inakuja Alexandrinus iliyo gunduliwa kwa karne ya 5 huko Alexandrie katika Misri, ina Agano la Kale na ya kushangaza, Agano Jipya inaanza na Mat.25:6. [Tazama elezo la biblia ya Frank Reisdorf-Reece]. Kwetu sisi, siyo kubahatisha. Tena, kwa hali ya 3, Vaticanus, ambayo asili yake haijulikane, isiyo na maana, haina 1 na 2 Timoteo, Filemono, Tito na Ufunuo. Imechungwa huko Vatican. Tunakadirisha kwamba maandiko haya ya mkono iliyo ambatana na waafrika na inayoanza na Mat.25:6 ni alama ya unabii. Na tazama ripoti ya wateolojia kama inavyo andikwa katika ile ile toleo, kwa ukurasa ule ule: “tafsiri ya kwanza ya kiprotestanti, ilikuwa ile ya Olivetan (1535), ikasahihishwa na Calvin (1550), na baadae [ikasahihishwa] na T. de Bèze na kutolewa na Kornelio Bertram (Geneva 1588). Tangu wakati ule, ilirekebishwa na Daudi Martin (1707) tena na Yoane Frédéric Ostervald. Leo kwa nafasi ya zile tafsiri zote ni tafsiri ya Louis Segond (Geneva 1874 na Oxford 1880), ile inayoitwa ya mtaguso (iliyo rekebishwa kwa 1926), na ile tunayo kadirisha kwamba ni aminifu sana kwa maandiko ya asili (origino), ni ile ya J.N. Darby”. Ninakamilisha kwamba tafsiri King Jams ilitafsiriwa na kundi ijapo Mungu hatumizii kundi! Na marekebisho kamili ya King Jams ikafanyika kwa 1881. Mbele ya kelele ya katikati ya usiku, mambo haya hayakujulikana, lakini sasa imejulikana, musifikirie! Muipokee kama amri ya Mungu. Mungu alisema katika Mat.25:6 na Ufu.12:14 kwamba ujumbe ndogo utakuja kwa kupeleka wachaguliwa mbali na uso wa Nyoka: mbali na makanisa hizo za kikatolika, protestanti, kiinjili na kibranhamisti,… mbali na roho mtakatifu inayo tenda katika makanisa hayo…mbali na hao wa Osborn, Ushe Praise, Morris Cerullo, Yongi cho, ...mbali na Next Generation Alliance, Carlos Annacondia, Paul Ayoh, Benjamin Boni, Jean-Baptiste Nielbien, Bernard Agré,...mbali na hizo maduka ya vitabu na vyombo vya habari viitwavyo vya kikristo,…mbali na hizo miungano na mashirikisho za makanisa,… [Mbali na vyombo hivyo vya uchawi viitwavyo biblia Louis Segond, King James, Tob, Martin, Scofield]… mbali na hao manabii wanao tembea duniani na, ujumbe huu ambao ni mabawa mawili ya Tai kubwa ya Ufu.12:14 inabidi iwapeleke wachaguliwa jangwani. Mujitenge nao! Kwani hakuna wokovu nje ya hii. Mutambue siku na ujumbe wake! Tuinamishe vichwa! Ninyi muliyo pale kwa mara ya kwanza, baada ya kusikia ujumbe huu, je! Kuna anaye amini kabisa na anaye penda kuikubali?... ikiwa ni hivyo, ainue mkono wake kwa upole!... inakubidi kuifanya kwa uhuru kwani hitaji letu siyo kwamba Mungu ageuze mapondo kuwa samaki! Ikiwa ataifanya, ingekuwa vizuri, kutakuwa samaki nyingi hapa, lakini samaki zilizo na mwenendo wa mapondo na baadae tuta pata wote shida… ikiwa anasema: nitanunua Biblia Darby lakini nitabaki ndani ya kanisa langu, mumwache! Munaona? Ni lipondo. Vema, kuna anaye penda kukubali ujumbe huu?... Na ikiwa hakuna, twende… [Ndl: mtu moja anainua mkono] Ndugu, Mungu akubariki! Ndiyo, ndugu pale! Dada, Mungu akubariki!... mwache mikono yenu juu ninapo waombea! Mungu akubariki pale! Mungu akubariki hapa… Bwana Yesu Kristo, ninaomba ili katika hii kujitolea, ushikilie nafsi hizi! Uamuzi wao utajaribiwa na shetani na hatuta kuweko kwa kuwashikilia lakini tunawaachia neema yako ya uungu!... na wakati tumemaliza ibada ya asubuhi hii, ninaacha kila ndugu na dada mikononi mwako kusudi, tunapo tengana kwa mwili, tuwe pamoja katika Roho moja na imani moja mbali na zambi mpaka tutakapo kutana tena! Bwana, utufanye wenye nguvu na kutupa ushindi juu ya zambi na juu ya shetani hata heshima, utukufu na ukubwa ikurudilie milele na milele, Amina!
kurudi kwa utaratibu