MAHUBIRI N°62

BWANA, WEWE NI NANI ?

(Ilihubiriwa siku ya tatu 30 mei 2007 huko Abobo,  Abidjan - Côte d’Ivoire
Iliandikwa na ndugu Akobé Benjamin toka kaseti
)



       Kuhusu kutokuanguka, nilisema kwamba ilibidi kuitazama kama muhuri, kwa namna ya stempu ; maana yake ni kwamba kabla nabii aingie kwa kazi, Mungu anaweka alama juu yake, anaandika juu yake : « asiyeweza kuanguka ». Hapo haizuru nini atafanya wala kusema, yeye ni asiyeweza kuanguka. Na Mungu anaweza kuruhusu mambo fulani ili atenge magugu na ngano lakini ile haiondoi kutokuanguka kwa yule nabii. Munaona ? Ni hivyo na ndio maana Biblia pia haionyeshi kamwe maisha ya nabii. Biblia inasema kwamba mfalme fulani alifanya yaliyo mema wala mabaya machoni mwa Bwana lakini namna gani inaweza kusemeka kwamba nabii fulani hakutembea katika njia ya Bwana ? Munaona ?

       … Mtu mmoja aliniuliza kama itabidi kungojea hapo hapo huyo mjumbe wa makesha ya nne. Sijui Lakini tambua kwamba Bwana akikawia, hakuta ngojelewa hata miaka kumi nyuma yangu ili kuwe nabii. Ukamilifu inahitaji hivyo. Kuhusu jogoo kuwika, kutainuka waisimaeli wengi watakao jionyesha katika ukristo kama manabii wala kama watu wanaotumwa [na Mungu], ni mambo haya yote ndiyo yatatambulisha jambo lililo la kweli. Pia nilipo hubiri juu ya siri ya kutokuanguka, wengi walisema: « Oh ! Nabii atafanya jambo hili wala jambo lile ! ». na wengine walisema : « Oh ! Ni kwa kutayarisha njia ya yule anayekuja nyuma yake kwa sababu waislamu wanakuwa na wanawake wengi » mufahamu kwamba sijui hata jambo moja kama vile ninyi. Ila Mungu peke anajua ! [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !].

       Sasa naanza kuelekea mwisho kamilifu wa ujumbe lakini ningali ninaamini kuendelea kwa huduma. Ninabariki Mungu kwa ajili ya wandugu na wadada ambao hawakuchoka kunisaidia na kunishikilia. Ninashukuru Mungu kwa ajili ya wachungaji na wahubiri wote katika Ujumbe huu. Pia, nilisema kwamba siku moja Biblia yangu ipewe kwa moja wao, ni kusema, kwa ndugu Bitty ikiwa mimi ndiye nitamutangulia katika utukufu. Na ombi langu ni kwamba yule yule malaika aliye niongoza katika mambo yote kwa namna sikuanguka kamwe kwa shauri, kwa matendo wala kwa Neno, awe pamoja naye. Siyo tu wahubiri lakini Mungu abariki pia mke wangu, mabinti zangu wawili, dada Coulibaly Sarah na kundi kubwa la tarehe 24 aprili 1993 ambalo sasa Neno limeonyesha. [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !].

      Vema, twaeni sasa Biblia zetu katika kitabu cha Matendo ya mitume. Matendo sura 9 na tusome mashairi tano za mwanzo. Nitaisoma ! Ni muhubiri ndiye anapaswa kusoma maandiko iliyo msingi. Munaona? [Ndugu Filipo anasoma Mdo.9 :1-5 : « Japo Sauli, akivutiwa tena kuhamakia na kuwatesa wafwasi wa Bwana, akamukwendea kuhani mkuu na kumuomba aandike barua kwa masunagogi zilizo Damasiki, kwa namna, ikiwa kutapatikana kwao wamoja wamoja wanao fwata njia ile, awapeleke Yerusalema, wanaume na wanawake wakiwa wenye kufungwa [kamba]. Na, alipokuwa njiani, alipokaribia Damasiki, na hapo nuru ikangaa toka mbinguni kama umeme wa radi kando yake. Alipoanguka chini, akasikia sauti ikimwambia :Sauli ! Sauli !  kwa nini unanitesa ? Na akasema : Wewe ni nani Bwana ? »]

      Munaona ? Hii ni mwanzo ya ukristo na sasa haitaweza kuwa tofauti na mwanzo ya uyahudi. Musa kwa ngambo ingine ! Paulo kwa ngambo hii hapa ! Malaika wa kijiti kisicho kinacho ngaa alikuwa ni Mungu mwenyewe na ngambo hii huko, malaika njiani Damasiki alikuwa ni Yesu-Kristo, Mungu mwenyewe. Munaona ?

      Musa alikutana na jambo la ajabu na aliona kile kijiti kisicho teketea. Na Musa alimuswali malaika aliyekuwa akimtuma : Wewe ni nani ili niweze kuwaeleza wayahudi watakapo niuliza ? Munaona ? Musa akasema : Ni kweli Mungu ni wa ajabu na sasa hiki kijiti siyo kazi ya binadamu lakini sasa wewe ni nani ? Na Mungu akamwambia Musa: «…Utawaambia wana wa Israeli hivi: NIKO amenituma kwenu». Kilicho pitika kule kwa mwanzo wa kanisa la Uyahudi, ikawa alama kwa wayahudi wote na sasa Paulo mwana wa kweli wa dini la uyahudi angeweza tu kuweka mambo yale kwa kazi. Munaona ? Paulo alisonga ngambo ya Damasiki akiwa mwenyi tumaini na gafla, nuru ikawaka kutoka mbinguni. Ile nuru ilikuwa yenyi nguvu kuliko upako wa makanisa zote za kikatolika, uprotestanti, kiinjili na kibranhamisti kwa jumla. Na ile nuru ikamwangusha Paulo kwa sababu wakati ule yeye alikuwa mpinzani wa Kristo. Ile nuru haiwezi hata kidogo kuangusha nafsi maskini inayo tafuta neema ya Mungu. Munaona ? Kila upako utakao angusha nafsi maskini inayo tafuta uponyaji au ufungulifu ni [upako] wa shetani ! [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. Mbele ya maadui au wapinzani wa Mungu, moto ikaitwa !  Mbele ya Sodomo na Gomora, moto ikaitwa ! Mbele ya hamsini za Ahazia, moto ikaitwa ! Lakini yeyote atakaye ita moto juu ya nafsi maskini inayo tafuta uponyaji au ufungulifu ni pepo katika mwili !  [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]...

      Basi Musa alifanya nini mbele ya huo ufunuo kuu ? Akauliza ile sauti iliyo kuwa ikizungumza naye : Bwana, wewe ni nani ? Amina ! Pia njiani Damasiki, hiyo nuru ilipo angaza, Paulo alianguka. Paulo alipoteza nguvu yote, alipoteza ufahamu. Alianza kuona kwamba ni mwisho wa maisha yake ! Paulo alianza kuona mauti lakini alipo pata tena ufahamu, alifanya nini ? Je ! alisema kwamba haya ni maajabu kubwa, lazima ni Mungu ? Hapana ! Je ! alisema kwamba lazima ni Mungu ameshuka mulimani Sinai ? Munaona ? Lakini aliuliza swali la kale na lililo la maana ambalo Musa na mababu walizoea kuuliza. Paulo alisema : nimeona utukufu wako kuu, nimeona uwezo wako kubwa ambao umeniangusha, nimesikia sauti ya ngurumo yako, …LAKINI WEWE NI NANI ? [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. …Ni kweli umenishinda lakini wewe ni nani? Munaona ? Ee Bwana wewe ni nani ? Tazama swali ambalo ulimwengu umelikosa. Kama leo kuna umati wa manabii, ni kwa sababu ulimwengu umesahau mambo haya. Tazameni duniani kote, ni wayahudi wangapi wamedanganywa na Osborn, Billy Graham, Morris Cerullo au Yongi Cho ? Hakuna, wao hawazubae. Munaona ? Ikiwa kuna balozi wa Israeli inchini mwetu, ni kwa sababu kuna hapa wayahudi lakini wangapi kati yao ni katika makanisa zetu ? Hakuna ! Munaona ? Kama Benny Hinn angelimwangusha muyahudi wa kweli, yule muyahudi angeli mulalamikia : ninaona kwamba wewe ni mtu mwenye uwezo lakini wewe ni nani ? [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. 

       Tazameni ginsi Yoane mubatizaji katika… Ninasoma Yoane 1 :19-23  : « na hii ndiyo ushuhuda wa Yoane, wakati wayahudi walituma makuhani na walawi toka Yerusalema, kwa kumuswali : Wewe ni nani ? Na akakiri, na hakukana, na akakiri : Mimi, si Kristo. Na wakamuuliza : Nini basi ? Wewe ni Elia ? na akasema : Si mimi. Wewe ni nabii ? Na akajibu : Hapana. Basi wakamwambia : Wewe ni nani ili tuwape majibu wale waliyo tutuma sisi? Unasema nini juu yako mwenyewe ? Akasema : Mimi, ni sauti ya yule apazae sauti jangwani ! ».  [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. Munaona ? Wayahudi walipo sikia yote Yoane alikuwa akifanya, je ! walifanya nini ? je ! waliwatuma makuhani na walawi ili wakwende kuona kama mambo wanayo yasikia ni ya kweli ? Hapana ! je ! waliwatuma makuhani na walawi kutazama kusitawi kwa huduma yake au wongofu mwingi na mavazi yake? Hapana ! je ! Waliwatuma wale makuhani na walawi kwa kuomba uhusiano au kumuomba Yoane Mubatizaji aingie katika shirikisho la makanisa ? Hapana ! Munaona ? Je ! waliwatuma hao makuhani na walawi kuona kama Yoane… Lakini Biblia inasema kwamba wayahudi walituma makuhani na walawi ili wamuulize yeye ni nani. [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. Yoane alisema : Mimi si Kristo ! Walisema : Ndio, lakini wewe ni nani ? Alisema : mimi si hiki wala kile lakini walisema : Ndio, lakini basi wewe ni nani ? Utuambie wewe ni nani ! Munaona ? hata kama Yoane angelisema : « Nina waaminifu elfu tatu ngambo hii, nina kusanyiko katika kila mji, nina makusanyiko huko Ufaransa, Ubeljiji, na… Nilifanya miujiza fulani, nina miaka hishirini ya zoezi, … ». Wale wayahudi hawange weza kuzubaa ! Ambacho wanatafuta ni kujua yeye ni nani ! [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. Je ! Biblia inasema kwamba kwa hizi nyakati, mahali hapa, mtu atafanya kile uko ukifanya vile ilikuwa kwa manabii wa Biblia ? [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. Munaona ? Ijapo walikuwa katika upotovu, ijapo katika Yoane 8 :44 ilisemeka kwamba wao ni wana wa shetani, lakini walipata hekima ya kumuswali Yoane yeye ni nani kwa sababu damu ya uyahudi ilikuwa ikitiririka ndani mwao. [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !].  Fanya  yote upendayo mbele ya muyahudi, ujulikane, ufufue wafu, dunia yote ikufwate, …atakuswali : WEWE NI NANI ? [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. Kwani ni kwa mambo haya ulimwengu ulikosa, ndio maana leo tuna manabii mia  wa mataifa. Hata ushuke katika kijiti cha moto, kama vile Musa, kila muyahudi au mwana wa Mungu, mdogo wala mkubwa, atakuuliza wewe ni nani ! ». Umwangushe muyahudi kwa makesha ya maombi, wakati angali chini kama vile Paulo, atakulalamikia : « ee bwana, wewe ni nani ? ». Lakini mwana wa shetani atasema : « Oh ! Tazameni mara ngapi yeye ni mwenye uwezo »... hata kama malaika akishuka ni hivi tu ! Munaona ? Katika Luka 1, mtu mmoja alimwambia Zakaria mambo mageni. Na Zakaria hakujua kwamba alikuwa ni malaika. Kama nyuma ya kusikia maneno yale angeuliza hapo hapo mtu huyu ni nani, hangekuwa bubu ! Munaona ? Ilikuwa ni kuchanganyikiwa kwa kuhani kama yeye.  

      Sasa tuisome katika Luka 1 :19 « Na malaika akamjibu akasema : Mimi ni Gabrieli ambaye ninasimama mbele ya Mungu, na nilitumwa kwa kukuambia… ». Haikuomba Zakaria atazame uzee wa mke wake ila tu  alipashwa kumwambia mtu yule : « maneno unayo niambia ni mageni ! mwanadamu hawezi kuyasema, basi wewe ni nani ? »  Lakini kuliko afanye hivi, yeye aliye muyahudi na tena kuhani, anazungumzia kuhusu uzee wake. Kwa namna Gabrieli akajibu swali lile akasema : « Mimi ni Gabrieli ninaye simama mbele ya Mungu ». Kama Zakaria angeuliza vile, hasingeli kuwa bubu ! Munaona. Muchunguze Biblia nzima na mutaona kwamba ni hivi. Hata wakati Yoane Mubatizaji aliwatuma wafwasi wake kwa Yesu, haikuwa kwa ajili ya kwenda kutazama kama habari za miujiza ambazo zilikuwa zikimufikia ni kweli ; lakini swali lilikuwa : WEWE NI NANI ? Hakika wewe ni Kristo ? Munaona ? 

      Na Yesu yeye mwenyewe katika Mt.16, alipo tazama wanafunzi wake, akaona huruma. Watu walikuwa wakimfwata kwa sababu alikuwa akizungumzia Mungu, Musa, sheria na manabii ; aliwaponya wagonjwa, alifufua wafu… lakini hata mmoja wa wafwasi hakusubutu kumuuliza yeye alikuwa nani. Kwa ngambo yao  yeye alikuwa mtu wa Mungu, na mwisho ! Na siku moja, Yesu akauliza swali hilo kwa nafasi yao. Nitaisoma katika Mathayo 16 :13-14 : « Japo, Yesu aliporudi kutoka miji ya Kaisaria ya Filipi, akawauliza wanafunzi wake, akasema : watu wanasema mimi ni nani, mimi, mwana wa mtu ? Na wakasema : wamoja wanasema : Yoane mubatizaji ; wengine : Elia ; na wengine : Yeremia au moja wa manabii. Akawaambia: Na nyinyi, munasema mimi ni nani? ». [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !]. Munaona? Hawajui hata kama wanamfwata nani! Ya muhimu kwao ni kuona Yesu anawazungumzia kuhusu Musa na manabii. Ni ile ulimwengu imekosa kwa leo. Munaona ? Kama munaona  T. L. Osborn, Yongi Cho, Benny Hinn, Ewald Frank, Morris Cerullo au Reinhard Bonke ni wa maajabu, kanuni ya kibiblia inaomba aulizwe: « Bwana, wewe ni nani ? je! Biblia inasema kwamba kwa wakati hii tunayo ishi kutakuwa mtu wa kizazi chako atakaye inuka kwa watu wa wakati hii na kufanya ile uko ukifanya ? Je !, uliitwa na kutumwa na MUNGU kama vile Musa, Paulo, au moja wa manabii ? …Tunaona miujiza yako yote, upako wako, ujuzi wako lakini wewe ni nani ? Utueleze wewe ni nani !...  ». [Ndl : Kusanyiko linasema :Amina !] . Wewe ni nani, bwana ?  Wewe, Bénoit XVI,… Nyinyi, wasimamizi wa makanisa,… Nyinyi wareverendi, Bishop,… Nyinyi, manabii wenyi upako,… Nyinyi munao unda makanisa, misioni na huduma, nyinyi ni wanani? Nyinyi munao vaa koti ndefu ndefu na zenye manyoya, nyinyi ambao manukato yenu nzuri mbele ya watu inanuka vibaya mbele ya Mungu kama arufu ya beberu yenyi manyoya mengi ya Danieli 8, ninyi ni wanani ? Nyinyi ambao matangazo na picha zenu zinabandikwa juu ya kuta kama mijusi, nyinyi ni wanani ? EE MABWANA, NYINYI NI WANANI ? Mujibu ninyi mabwana ! Nyinyi ni wanani ?       

       Utuambie wewe ni nani kusudi tuwaeleze wale watakao tuuliza. Je !, wewe ni Mathayo 25 :6 iliyo fanywa mwili ? Wewe ni Kristo ?  Wewe ni nabii ? Wewe ni nuru ya ulimwengu ? Je !, ni wewe unazo funguo za ufalme wa mbingu kwa wakati wa leo?... Basi wewe ni nani bwana ? Utuambie wewe ni nani ? … O Mungu ! Asante na heshima iwe kwako milele na milele   [Ndl : Kusanyiko linasema : Amina !].

       Tusimame wima katika roho ya maombi… Ikiwa uko pale kwa mara ya kwanza, au ya pili au hata ya tatu na bado hujakubali ujumbe huu, nyosha tu mkono kwa kusema kwamba sasa unaukubali!... 

        Na magharibi ya leo, kisha kusikiliza mahubiri haya ikiwa unaamini kwamba mimi ni nabii anaye pashwa kuja kwa kizazi chetu kama inavyo andikwa katika Mathayo 25 :6, nyosha mkono wako na omba yote unapenda kwa nguvu ya ile imani ! [ …] 


Tuma ukurasa huu kwa rafiki

kurudi kwa utaratibu

www.matth25v6.org - Copyright © Aprili 2007
Kisheria Deposit ® All rights reserved