MAHUBIRI N°6

MAHUBIRI JUU YA MATHAYO 25: 6 (2)

(Ilihubiriwa jumapili asubuhi 22 desemba 2002 huko Locodjro, Abidjan, Côte d’Ivoire)



      Tunajua kutoka Mat.24:27 kwamba Injili ilitoka Asia, mashariki pamoja na Paulo na mitume wengine. Rangi ya jua asubuhi ni kimanjano na watu wa Asia kwa mfano ya watu wa kichina, ni wa rangi ya kimanjano. Kiisha jua, Injili ilifika Ulaya mahali jua inageuka nyeupe. Kulikua watu wakubwa wa Mungu kama mtakatifu Martin de Tours, Ireneo, colomban. Na hapo, tunajua ya kwamba wanao ishi Ulaya ni watu wa rangi nyeupe. Kisha jua ikaelekea Mangaribi pamoja na John Wesley huko Uingereza mpaka ikafika Mangaribi ni kusema Amerika. Jioni jua inapo karibia kulala, jua inageuka nyekundu. na wakaaji wa kwanza wa Amerika ni watu wa rangi nyekundu. Na kulikuwa William Branham pamoja na nuru ya jioni. Na William Branham alionyesha ya kwamba alikuwa na damu ya wahindi kwa muke wa babu wake. Na sasa Ewald Franck, mzungu, ananenea kelele ya katikati ya usiku. Na tunajua kwamba nyuma ya wakati ya jioni ni usiku, weusi, Afrika kabla ya kurudi tena Mashariki pamoja na washuhuda wawili wa Ufu.11. Hata kwa hali ya mwili tunaona weusi juu ya vituo vya juu duniani. Na hata kwa mara ya kwanza, tunaona mtu mweusi kama mkubwa wa UMOJA WA MATAIFA. Na hizi miaka kumi za mwisho, tuliona waamerika weusi wakijipendekeza kwa Afrika na hata kutafuta asili yao kamili. Kwa kutembelea Afrika, Mungu atakumbuka watoto wa Toussaint Louverture, wa Wilberforce, wa Martin Luther King na wengine.

    Wakati Frederik de Klerc, mzungu na Nelson Mandela aliye mweusi, walishikana mkono mkononi mbele ya jamii ya kimataifa kwa 1993 wakati hao wawili walipokea tuzo (Nobel) la amani, ilikuwa mwisho ya ubaguzi wa rangi na ya wakati moja. Ilikuwa alama ndogo iliyoficha upande wa muhimu sana wa kiroho.

    Na kama Mat.25:6, katikati ya usiku kelele itapiga, mahubiri fupi itakayo shitua na kuamsha mabikira wa makesha saba. Na hiyo uamsho itapeleka Bibi Arusi kwa kuchukuliwa. Yesu-Kristo atatembelea Afrika. Mwezi na nyota zitangaa. Isaya 30 itatimia. Na manabii wengi wanakubaliana kwa kusema kwamba uamsho itatokea Côte d’Ivoire. Na kwao waliyo wapole wa moyo na wa roho, kwa wale wanao ngojea kuchukuliwa ya watakatifu, hii siyo tena unabii lakini uhakika. Na wakati Mungu yuko kwa kazi kila tukio inashiriki kwa wema. Kwa nini hiyo mgogoro, hiyo harakati upande ya Abidjan? Hiyo ni mvuto gani? Kumbuka katika Luka 2:1-7, mfalme Kaisari Augusto akaomba kila mtu ajielekeze katika mji wake wa kuzaliwa ili jina lake liandikwe. Kwa nini? Yeye mwenyewe hakujua lakini ilikuwa ili Yesu azaliwe Betelehemu kusudi unabii zisichanganywe. Tulisikia, tulikuja kutazama na tumeona kupitia maandiko matakatifu kwamba huyo muhubiri ni Yule aliye tuahidiwa katika Mat.25:6 na ni yeye inatubidi kumfwata…

       …kelele ya katikati ya usiku inashika msingi mkuu wa Biblia lakini kwa atua tunayo ifikia, kwa mchaguliwa wa Mungu, ile inakuja kuongezwa kwa yale anayoijua tayari. Wakati watoto wa shetani wanapo kokota kamba pamoja na mustari ya mawazo, wachaguliwa wanajiweka watawala wa mambo. Ninashikilia nikisema hivi, kuhusu rangi nyingine za ngozi: Mungu amewakumbuka wajukuu wa wajukuu wa Simoni wa Kurene. Wale ambao bado hawaja tawala wengine wala kutawala wanapokea neema ya Yule asiye na ubaguzi na inabidi dunia nzima itambue hayo!

    Tukamate sasa Biblia katika…nitawapatia mashairi mutakazo zisoma kwa ukimya nyumbani, hatuna wakati ya kutosha asubuhi ya leo. Kamata Ezekieli toka kipindi cha 29 mpaka kipindi cha 32 kisha Isaya toka kipindi cha 18 mpaka kipindi cha 20 kisha Yeremia 46. Tena Ezekieli 21:1-5 kisha Hosea toka kipindi cha 7 mpaka kipindi cha 12, na kazalika……

      Hizo unabii zote zinanenea Afrika iliyo mfano wa Misri, Etiopia na Libia. Tusome Isaya 19:23-25… Bwana atamubariki akisema: Ubarikiwe ee Misri taifa langu na Israeli uriti wangu na tunajua ya kwamba Misri ambayo Biblia inazungumzia siyo hii nchi ya kiislamu tunayoijua lakini Afrika nzima. Tazameni mustari wa 2! Nitaamsha mumisri juu ya mumisri na watafanya vita… mji juu ya mji, nchi juu ya nchi! Munaona? Tunaona utumwa, mateso ya weusi katika Isaya 20:4 vijana na wazee, watupu na miguu yao pasipo viato na viuno vyao pasipo kufunikwa kwa haya ya…Afrika. Hata kabla ya karne ya XV, kulikuwa kuchukuliwa kwa waafrika kuelekea Irak (Babiloni ambayo ndani mwake kuna Asuria) pale Basra kwa karne ya IX. Juweni kwamba wakati Mungu alipokuwa akisema kwa wakati ule hakuwapo wala Burkina, wala Zimbabwe, wala Kenya, wala Afrika ya Kusini, na nyuma kukawa  kutoka na tunajua namna gani Kwamé Nkrumah* alionyesha kwamba wa Ashanti walitoka Misri na nyuma[tena] rais Bédié alionyesha pia kwamba wa akan walitokea Misri kwa kupitia Ghana ya wa Ashanti. Na tunaweza kuona kwa wa akan kabila ya wa Houphouët, falme zinazo fwatana na mtindo wa kimisri pamoja na kiti cha ufame, mapambo ya zahabu, uwanja wa kifalme, taji ya ufalme, gongo la mfalme,… pyramidi ya viwango nne kwa mfalme wa indenié na pyramidi ya viwango viwili kwa wa nana Yéeboua, mfalme wa waabron. Wa akan ni kabisa uzao wa Misri. Na katikati ya Akan kuna makabila kama Abidji, waliyo wachache sana ambao hesabu ya vijiji vyao ni kumi na mbili kama kabila kumi na mbili za Israeli. Kabila la Abidji linafanana lile la Ashanti mpaka kupitia hata majina bure. Na moja ya vijiji vyake kumi na mbili inaweka shule kubwa ya teolojia ya kusanyiko za miungu na hicho kijiji ndogo, Katadji ni changu na kina hesabu ya vizazi saba vya miaka saba. Dipri ya Abidji inaelezwa katika 1Wafalme 18:28-29. Na nilizaliwa wakati malaika waliimba huko Katadji karibu asubuhi na inajulikana kule. Na tendo la kuzaliwa kwangu linaonyesha saa kumi na mbili ya asubuhi. Wabranhamisti wanasema kwamba ni huko Sikensi ilifanyika lakini washuhuda wa Katadji wanaleta maelezo juu ya wimbo uliyo tokea katika kijiji ndogo chetu upande wa kijiji cha chini na iliyo rudi upande wa kule lakini vijiji vya pembeni ambavyo ni Elibou na Sikensi, kwa km tatu karibu na Katadji walisikia tu wimbo wa kimbinguni. Na siamini kwamba ile inatokana na kuja kwa ujumbe wa jioni huko Côte d'Ivoire kama wanavyo sema wamoja. Ila tu ikiwa ilifanyika pia katika nchi nyingine wakati ujumbe wa jioni ilifika kule. Siamini pia kwa masemi ya kusanyiko za miungu wanao shikilia kwamba ni kwa sababu ya wepo wa shule yao ya teolojia huko Katadji kwani hiyo shule ilikuweko miaka nyingi sana kabla kufanyika kwa tukio hili la mahajabu. Sasa, kumbuka siku ya kuzaliwa kwangu, wazazi wangu walikuwa Elibou, iliyo kwa mwendo wa saa moja. Na ni pale nilizaliwa upande wa saa kumi na mbili ya asubuhi. Mara moja tulirudi Katadji. Elibou maana yake nini? Kijiji cha Elia. Muite haizuru Abidji Fulani, akasema tofauti halafu mimi ni nabii ya uongo. Munaona? Kijiji cha Elia! Mtu ambaye Roho ya Elia itatulia juu yake atazaliwa pale katika mji moja huu wa Sikensi.

      Vema, tusome Ezekieli29:12 na 30:26… nitawasambaza wamisri kati ya nchi… juu ya uso wa dunia. Ô! Kumbuka Matayo 27:25 "…damu yake iwe juu yetu na juu ya watoto wetu" na kwa mwaka 70, jeshi la waroma likiongozwa na jemadari Titus liliwaua wayahudi huko Yerusalemu, ilikuwa utimilifu wa:…juu yetu”baada ya miaka 1900 nyuma zaidi, wayahudi wakashambuliwa popote duniani na kuuawa kwa mfano na Adolf Hitler huko Ujerumani, na Yosefu Staline huko URSS, na Benito Musolini huko Italia, Poland,…pembe kumi za Ufu.17:13 zilizo na mpango moja na kanisa katolika. Sawasawa kanisa katolika iliwaua mamilioni ya waprotestanti, vivyo hivyo hizo mataifa kumi zilisimama kuwaua wayahudi! Ilikuwa utimilifu wa: …juu ya watoto wetu” na tunaona hao watoto hawakuwa huko Israeli. Popote walikwenda, hii neno iliwafwata na ni hivi hata leo! Katika mwanzo Mungu alitumika na taifa lililo teswa sana kuliko wote duniani, kwa mwisho, Mungu anatumika na rangi ambayo iliteseka sana kuliko wote duniani. Ndiyo maana siamini kwamba mtu anaweza kuwa mbeba bendera wa nchi ingine hata ikiwa anaishi kule.

       Mungu hangeweza kutumizia mumisri kwa kutoa Israeli kule Misri hata mweusi kwa kuwatembelea wazungu. Ndivyo Mungu anatenda [kila mara]. Siyo kusema weusi hawastahili. Na hata siku moja Mungu hakuruhusu William Branham kwenda kwa Afrika ya weusi na kwa wayahudi. Kwa nini? Kwani kila mmoja ana ahadi yake na wakati yake ya kutembelewa. William Branham alikuwa njiani kwenda Israeli lakini alipo fika Misri Mungu alimuzuia. Na Yesu-Kristu mwenyewe katika huduma yake hakuruhusu wanafunzi wake kwenda kwa wasamaria na mataifa.

      Mahubiri haya ni tu kelele ya Mat.25:6. Na ni msingi wa mahubiri ya uamsho. Wamoja wananiita mpinga Kristo, mtume wa shetani, mahubiri nivaquine, wengine wananilaani na wanatoa unabii ya uovu juu ya maisha yangu lakini ninafurahi kwani tayari watu wanakuja na kuamini pasipo juhudi yetu. Biblia inasema nini? …na wote waliyo ahidiwa uzima wa milele wakaamini.” Matendo 13:48. Amina! Katika siku chache wahubiri watakwenda toka hapa pamoja na [hii] Roho moja wakihubiri hata yale ambayo bado sijahubiri. Mungu ataanza kusimamisha watu walio na misemwa ya ukali sana kuliko mimi. Ilikuwa hali ya Mutzer na Calvin ambao waliona mahubiri ya Lutheri ni“ya kike sana. Kelele ya katikati ya usiku itakuwa na sauti za kusikilika mbali. Sauti inaposikika mbali inapoteza sifa zake lakini kilindi na shabaha  zinadumu.

     Vema, Mat.25:6, tunaishi katika wakati ingine ya historia ya wokovu. Siyo tena wakati ya kujenga majengo makuu ya kidini, mapambo, viombo vya kuleta hewa bora, vyombo kubwakubwa vya kutoa sauti. Siyo tena muda ambao mtu wa Mungu anafikiria nyumba kubwa, magari,…lakini juhudi zote, mapato yote inakwenda wima katika mwendo wa kutapanya hii ukweli kwa sababu ya uamsho. Na hakuna anayeweza kutumikia Mungu isipokuwa yeye ni sauti ya mbali ya ile Mungu iko akifanya hapa. Ndio maana mimi sikubaliane na wainjilisti wa kibatisti, foursquare, na wengine… Ninawapa ninyi angalisho! Musiwe zingine shamba za mapambano juu yetu. Tai wanapo lia, kunguru wakae kimya. Unapo hubiri muislamu au mukatolika na kumupeleka katika kanisa la kibatisti au pentekoste, basi umefanya nini? Hapo unabadilisha tu mfungwa chumba katika gereza. Ni mzunguko wa ukuta moja tu ya shetani. Wewe ni sauti ya ugomvi juu ya yale Mungu iko akifanya!

  Mat.25:6-7, ...wakati ya wahubiri wasujaa imetimia na ni kivuko kwa imani ya mitume. Wahubiri watakwenda popote katika kampeni, miji na nchi  kwa kuwafunulia watu wote kwamba roho zinazo tenda katika makanisa hizi za katolika, methodisti, injili, pentekoste, batisti, foursquare, katika hizo makanisa na mahuduma za moto,…siyo Roho ya Mungu lakini roho ya shetani, kwamba hao manabii ni tu wachawi wenye hila, ni wamoja na wafumu  Gbahié, Zérédji na wengine; kwa kufunua kwa kweli sura ya mashauri na shirikisho za makanisa zilizo vyombo vya siasa, vitunga vya maskini. Mungu si maskini! Na wakati mutu wa kisiri ambaye yeye bado hakunawa mikono yake anajiingiza kwa vitu vitakatifu, ni hatari na ni pia hali ya Soumah Yadi, murosikrusia na mtu wa siasa kisha tu kuongoka katika kanisa moja na anayejiweka kama malaika wa Mungu ijapokuwa angali prezidenti wa chama cha siasa. Munaona?

      […]Nchi zinazo jidai kwamba siyo za kidini bila hata hali moja ya mambo ya uungu,… na sielewi hiyo kusukumwa ngambo na ngambo, kwanza manabii wachawi. Maskini wanao jificha sura wakikwenda hata kujifanyia sanamu ya kutakaswa baada ya kufa kwa makanisa na huduma. Kwa kukubaliwa na kupata neema, makanisa na wanamemba wao inawabidi kuingia katika hizo miungano za makanisa na hiyo, kwa kulipa 50.000 F kwa makanisa na 10.000 F kwa watu wa Mungu bila kuhesabu kuwapigia magoti wanasiasa, viama vya siasa, ma mea za miji na vingine vituo. Katika barua moja ya 05/11/2002, N°AN/CNEPE-CI/201/02, shauri la taifa la makanisa [Cnepe-ci] linaomba kusaidiwa na [pesa] zaidi ya milioni moja kwa ofisi ya mea ndogo ya Attécoubé ili waombee nchi yao binafsi iliyo katika vita,… nchi yao wenyewe! Kati yao wanafanya ushindani wa shule za upekee, maduka makubwa, kazi katika mabenki na ma jamii, magari za kusafirisha, taxi, makanisa za biashara… Na jumapili, wote wanageuka malaika. Makanisa zinaoza! Viongozi wao wanafikiria tu ma gari, manyumba kubwa-kubwa, kunona, wavae viatu na koti za bei ghali ijapokuwa katika zile makanisa moja, kuna maskini. Munaona? Mbwa mwitu na mchungaji hawatazami wana-kondoo kwa namna moja. Namna gani Mungu anaweza kuwaachia ma mbwa mwitu mlango wa zizi? Na ikiwa wao ni wachungaji wa kweli, namna gani wanaweza kuacha mlango wa zizi na kupatikana katika nyumba ya kifalme. Hao aki na Luis Palau, Franck Alexandre, Jim Lassiter, Hamsa Eichler, Samuel René Sirat, Nichiko Niwano, Konrad Raiser, Elio Toaff,... wao ni tu mapepo waliyo poromoshwa katika mili za watu. Siyo tena kwa Roho Mtakatifu lakini kwa barua ya mwanamemba wa shauri la makanisa ndipo wanamtambua mtu wa Mungu. Hicho kikundi cha watu wenye tabia mbovu wanatembea kwa uhuru na wale wanao wafwata. Labda nionyeshwe tofauti, hii shirika ni umbo la shetani na kuzimu haichoki kupaza sauti juu yenu: “Hukumu! Hukumu! Hukumu!”. Ninyi, makuhani wenu, na wanamemba wenu, mutakwenda kuzimu. Mumeharibu dunia, Mungu atawaharibu ninyi! Na tayari ninabaki fimbo ya chuma na upinde unao kokotwa juu yenu.  Ee Mungu! Simamisha wahubiri wanao nena kwa ugumu zaidi kwa msingi, pamoja na nafsi za chuma, na wenye mahubiri ngumu ambayo hakuna awezaye kuyafazaisha na ambao kwao inawaka Roho, moto, na maneno ya uzima wa milele. Imeandikwa: “mumupe Kaisari yaliyo ya Kaisari”, lakini Kaisari mwenyewe amekuja kukaa ndani ya makanisa kama mungu, akivaa ngozi ya kondoo, akitumia Kristu kuliko kumtumikia. Hawatafuti tena kukata vichwa lakini wana chuna nafsi na wanapora kwa jina la Mungu. Wamekaa juu ya viti vya enzi wakitangaza kwamba wao ni wakuu wa makuhani ni kusema rais (au presidenti) wa makuhani wote wa katolika, batisti, metodisti, kusanyiko la miungu, maisha kilindi, mashahidi wa Yehova,… mkuu wa makuhani= DUX CLARIV’S inayo leta kwa hesabu ya waroma 666 iliyo hesabu ya cheo, jina ya makufuru ya mpinga Kristo. DUX CLARIV'S (mkuu wa makuhani), kwa namna ya kawaida inaimarisha kwa wapagani: rais wa shauri la uongozi. Ni kusema mkuu wa walio na uongozi au wanao ongoza shirika au jamii. Lakini, 1Yoane2:18 alisema: «watoto, ni saa ya mwisho; na kama vile mulivyosikia kwamba mpinga Kristo anakuja, hata sasa wapinga Kristo ni wengi». Mulisikia kusema kwamba kutakuwa na papa lakini sasa kila kanisa ina papa wake, rais wake… Kuna mapapa wengi wa makanisa… wapinga Kristo. Wote ni watawala, wafalme, maliwali,… hata zikiwa ndogo ndogo makanisa ambazo wanazisimamia. Kwa hesabu ya waroma, kuna: D = 500, X = 10, C = 100, L = 50, I = 1, V = 5. Hivyo, DUX CLARIV'S inaleta 666. Lakini, papa anabaki VICARIV’S FILII DEI inayoleta pia 666 na ambayo maana yake ni: msimamizi wa mwana wa Mungu au aliye kwa nafasi ya mwana wa Mungu. Na, namna inavyosemwa katika Ufu.13 na 17 tunaona wazi wazi kwamba makanisa protestanti, za kiinjili, ma misioni na huduma ni binti, ni kusema picha ya kanisa katolika ya Roma na sasa warais (prezidenti) wao ni tu picha ya papa aliye Roma. Ninaisema bila kusahau wabranhamisti, mwanamke mzungu-nusu katika gari kubwa la kiaskari.

      Munaona? Hizo ni huduma gani zinazoitwa kuhani mkuu wa parokia, reverenti, prezidenti (au rais), kardinali, papa? Na kwa namna ya kidini, neno reverenti ni kusema: anaye heshimiwa au kuabudiwa. Wakatolika wanasema kwamba wanaheshimu Maria na munaona vema kwamba inaimarisha: kuabudu. Kwa wapagani, maana yake: muheshimiwa, au mwenye heshima Fulani. Ile ambayo mchonga sanamu anafanya kwa miti, ni ile shetani anafanya nanyi, akichora ma sanamu, miungu, na kuwapa mamlaka ya kusema kwa jina lake kama André Kouadio. Na reverenti wa Côte d’Ivoire Dion Robert, yeye si zaidi kuliko mask yakuba. Ni mfanya kazi wa zamani wa kabila la Dani na la Efuraimu ambao majina yao ziliondoshwa juu ya utaratibu wa makabila kumi na mbili katika Ufu.7 kwa sababu ya bidii yao ya kuabudu sanamu, tangu Yeroboamu katika 1wafalme 12:28-30. Angalieni pia Hosea 4:17…

      Mapepo hawakupoteza hata moja ya yale walio kuwa nayo kabla Injili ifikie Afrika. Walitoka tu katika maji, pori na mwitu takatifu, mifereji, pahali pa juu, milima, asili,… kwa kupatikana sasa ndani ya makanisa. Na nguruwe na ndege wachafu na wabaya sana, wale majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia wataziabudu kama imeandikwa katika Ufu.13:8. Katika Isaya14:13-14, marais hao wa makanisa, malaika hao walio anguka walipenda kupanda juu ya kiti cha enzi cha Mungu ili waabudiwe kama Mungu. « Nawe, ulisema moyoni mwako: nitapanda juu mbinguni, nitapandisha kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu, na nitakaa juu ya mlima wa kusanyiko, kaskazini kati. Nitapanda juu ya urefu wa mawingu, nitafanana na Mujuu sana ». halafu kukawa na vita, na wakaporomoshwa juu ya dunia kama inavyo andikwa katika Ufu.12:7-9. Na kwa mwisho wa nyakati, mapepo hao wanapokamata hali ya binadamu, wakaja kujiweka juu ya makanisa kama miungu, badala ya kutubu. Na tunaona tena kwamba watatupwa kuzimu: wao, makanisa yao na manabii wao.

      Nilikuwa mpagani na nilipata mwito kisha nikapata tume. Sihubiri basi ninayo wazia kuwa kweli au mawazo lakini ninasema yaliyo ya Yesu-Kristo. Sijaingia hata shule moja la uchungaji, sijasoma hata kitabu kimoja cha teolojia. Ni tofauti na Yule anayesikia ndani mwake bidii au anaye ona kifo cha kiroho ndani ya kanisa na anaanza kufanya kitu Fulani. Pale, ni makosa na hata ni zambi kwani ile haionyeshe kwamba una huduma, au ni wewe unaye paswa kuifanya! Si kwa sababu mwalimu anaona wachezaji wakicheza vibaya ndipo atajiingiza ndani ya uwanja. Hapana! Haizuru nini utafanya, miujiza, nafsi, haukubaliwi. Hata ukiingiza goli nyingi, ni bure. Hata hapo wewe unakuwa hatari kwa wachezaji wako. Mungu hawezi kutambua kazi na juhudi ya mwenyi hakutumwa naye. Na ikiwa kuna atakaye mfwata mtu kama huyo, ni kwa upotevu wake. Ninapo hukumu makanisa yote hata wabranhamisti, ni neno la nabii, ni “Ndivyo asema Bwana” na siishakie. Munaona? Na ninapenda kwenda tena mbali zaidi nikisema kwamba… Biblia inasema: « … Na Mungu akapendezwa na Abeli na sadaka yake; lakini kwa Kaina na sadaka yake, hakupendezwa...». Munaona? Kuna, kwa upande moja, mtu na kwa upande mwingine, sadaka ya Yule mtu. Kuhusu Abeli, Mungu akamkubali katika mawazo yake kabla dunia iwekwe misingi na kwa hiyo akamkubali na akalazimishwa kukubali sadaka ndipo akamfunulia ile sadaka. [Kusanyiko inasema: Amina!]… Siyo kufanya siku makumi saba za kufunga chakula, kutumikia Mungu kama tembo, lakini yote inatokana na ukubwa wa Mungu. Kabla kuwekwa msingi dunia Abeli tayari alikubaliwa na baadae katika shamba la Edeni, yeye na sadaka yake… [Isiyo rikodiwa]. 

      Kwa karne ya XVI, Martin Lutheri alipokuwa akisukumana na ukatolika, rafiki wake Erasme akamwacha, akiona kwamba mafundisho ya Lutheri ni “ya kutukana sana na ya uchokozi” lakini Lutheri alidumu sana kwani aliona kazi ya Mungu ni ya damani kuliko damu yake. Badala ya kuangalia katika Biblia au kupiga magoti, watu wanapendelea kugeukia upande wa wachungaji na wengine. Kwa upande wangu, nikikamata mbingu na dunia kama washuhuda wangu, mbele ya Mungu na malaika wake watakatifu, na mbele ya watu, nimetia njia, kweli na uzima mikononi mwenu. Muifanye namna munavyo pendezwa!


Tuma ukurasa huu kwa rafiki

kurudi kwa utaratibu

www.matth25v6.org - Copyright © Aprili 2007
Kisheria Deposit ® All rights reserved