… Mabikira kumi walitwaa taa Paulo alipo wachumbia kwa Kristo. Na ile Neno moja, ile taa ilibadilisha hali na hatua kwa kila nyakati, kama farasi ya Ufu.6. Kila mjumbe anakuja na mafuta lakini kwa kila usingizi, taa zinazimika kwani mafuta, Roho inasogea, inawaacha… kwa shairi la 7, siyo "wakaamka" lakini "wakasimama" kwani mabikira wenye busara hawakulala kamwe.
Wandugu, tunapenda nguzo la moto kwani picha ya moto, hata iwe kubwa kadiri gani, haita tuchamusha! Hatutaki shuhuda za kihistoria ya uponyaji, miujiza na ya ufufuo. Dunia haihitaji mambo haya. Sina heshima hata kidogo kwa zoezi ambazo zimepita miaka 40 au 2000. Waebrania 13:8 inatimia siku zote! Dunia inahitaji Yesu aliye hai. Munaona? Na tayari tuna ushuhuda mwingi ya uponyaji na ya ufungulifu alisi. Tuko tukielekea kwenyi miujiza kuu, hadi kufufua wafu. Yote Yesu-Kristo alifanya alipo kuwa katika mwili, inabidi aifanye tena ikiwa yeye ndiye Malaika na Mwana Kondoo, pia [kama yeye ndiye] Ujumbe wa tarehe 24 aprili 1993…
Tutwae Biblia zetu katika 1 Wafalme 19:1-13 na tusome… kwa sababu asubuhi hii, nabii aliye tumwa na Mungu anataka kusema na dunia. Ningependa nihubiri juu ya mashairi 9 hadi 13 lakini katikati ya… Napenda nisome mashairi 11-13: " Na Bwana akamwambia Elia: simama na uende mlimani mbele ya [uso wa] Bwana. Na tazama Bwana akapita, na mbele ya Bwana upepo kubwa ulikuwa ukipasua milima na kuvunja miamba: Bwana hakuwa katika upepo. Na kisha upepo, tetemeko la inchi: Bwana hakuweko katika tetemeko la inchi. Na kisha tetemeko la inchi, moto: Bwana hakuwa katika moto. Na kisha moto, sauti tulivu na ya siri. Na ikawa wakati Elia alipo sikia sauti hiyo, akafunika uso wake katika kanzu lake, na akatoka na akasimama kwa mlango wa pango."
Vema … Elia, nabii wa Mungu alikuwa mwishoni mwa huduma yake na kama Musa, Mungu akampandisha juu ya mlima ule ule kwa kumwonyesha mambo yatakayo kuja. Katika Kumb.34:1-3, Israeli alikuwa bado angali ngambo ingine ya Yorodani wakati Musa alipoona katika maono Kanaana iliyo gawanywa kwa wana wa Israeli. Tena Musa, nabii wa Mungu akaona katika ono, vita itakayo kuja. Musa aliona vita, udanganyifu, ujanja na makosa ambayo ndani mwake wakanaana watawasukuma wayahudi. Musa aliona pia makuhani saba wa Yosua 6 kwa nyakati saba za kanisa, na Kelele ya katikati ya usiku kwa shairi la 5. Musa aliona Mungu akilinda Israeli kwa nabii Yosua kama inavyoandikwa katika Hosea 12:14: "Na kwa nabii Bwana akapandisha Israeli toka Misri, na kwa nabii Israeli akachungwa". Hivyo, katika 1 Wafalme 19, kwa mwisho wa huduma ya Elia, Mungu akampandisha juu ya ule mlima kwa kumwonyesha udanganyifu, jeshi kubwa la Mungu ambalo ilibidi lije kuwajaribu wanao kaa duniani. Nyuma ya ule udanganyifu kutakuwa sauti tulivu na ya siri ambayo itaweza kusikika.
Ule udanganyifu kuu ulionwa na Bwana Yesu mwenyewe. Kwa mwisho wa huduma ya Yesu, katika Mt.24, akapanda juu ya ule mlima na akaona kunyakuliwa kunako sura ya 25. Akiwa juu ya ule mlima, akaona mihuri saba na Mathayo 24:24 ambayo ni 1 Wafalme 19:11-13. Katika Matendo ya mitume 20:17-38, kwa mwisho wa huduma ya Paulo, Mungu akamunyanyua juu ya ule mlima na alipoona ule udanganyifu, akalia. Kwa mwisho wa wakati ya unabii wa miaka mitatu na nusu iliyo pewa kwa ule ujumbe, ile siri ikafunuliwa.
Na manabii wote wa kweli waliona ule udanganyifu mkuu ya mwisho wa nyakati: manabii wa Baali wanao vaa koti wakikaa juu ya viti vya enzi kama viti ambavyo Ahaba aliwapa na pahali pote, mabinti wa Yezebeli, wa uzao wa nyoka walikaa kando yao juu ya viti vya enzi vinavyo fanana mbele ya kusanyiko zao, wale ambao majina hazikuandikwa ndani ya kitabu cha uzima cha mwana Kondoo kabla dunia kuwekwa msingi.
Sasa, turudi kwa huu usomi tukufu wa 1 Wafalme19:11-13. Munaona? Hatua tatu na baada ya maneno haya ni sauti ya siri, siyo baragumu wala sauti nyingi lakini sauti moja! Musa aliisikia kwa hali ya kelele na ni mtu ndiye alipashwa kuionyesha, yaani Yoshua. Yesu-Kristo akaisikia kwa hali ya kelele katika Mt.25:6 na huduma ya Ufu.12:14.
Katika Sabino Canyon, William Branham akasikia ile sauti ikisema na mtu mwingine juu yake [Muhuri wa 7, Kifungo.191-192 au mahubiri: 30]. William Branham akasema: "nilikuwa nikiangalia, na tazama ngambo ingine kulikuwa mahali moja iliyo fananishwa na sanduku. Halafu nikaona kama ile nuru ilikuwa ikisema na mtu mmoja juu yangu, ile Nuru munayo iona pale juu ya picha". Munaona? Lakini hajui kwamba ni ile iliyo semwa na ile Nuru ndio aliyo isikia katika lugha isiyo julikana. Kwa mwaka 1993, nilisikia ile sauti lakini sikuona mtu, kisha nikaisikia katika lugha isiyo julikana lakini ninyi munaisikia wazi wazi kwa sababu ahadi ilikuwa kwenu. Ni nini iliyo kuwa ikipitika ndani ya ile upepo, ile tetemeko la inchi, ile moto na ile sauti ya siri? Maana ya neno "Tulivu" ni "siri". William Branham alisema: « … Kutakuwa kelele, lakini siyo kati ya wasiyoamini: itakuwa siri. » [Kifungo 134 «Wakati na alama ya muungano » 18 Aogusti 1963, Branham-Maskani Jeffersonville USA]. Munaona? Siri. Hiyo ni nini? Mungu alikuwa akimfunulia Elia udanganyifu mkuu ambao ulikuwa ukingojea uzao wake wa kiroho kwa nyakati za mwisho. Ni pia mihuri saba. Na ile sauti ilikuwa ndani ya ngurumo saba na ilipashwa kutiwa muhuri hadi nyakati za mwisho ili ifunue huu udanganyifu. Ufunuo wa ngurumo saba hauwezi kufikia mwisho kabla ya kufunua wabranhamisti. Munaona? Lutheri alipo kuwa akihubiri, ilikuwa ni ngurumo saba. William Branham alipo kuwa akihubiri, ilikuwa ni ngurumo saba. Na itabaki tu ngurumo saba mpaka siku Bwana atakapo rudi.
Hizo hatua tatu zinafwatana hasa na udanganyifu ulio kati ya wakati wa jioni na katikati ya usiku. Ufunuo unasema kwamba Elia, katika pango, akasikia sauti ambayo ilikuwa ikisema na mtu mwingine juu yake kama ilivyo kuwa ndani ya muhuri wa 7. [Kusanyiko linasema: Amina!]. Ile sauti tulivu na ya siri ni tofauti na sauti iliyo muuliza nini alikuwa akifanya pale. Sauti ya kwanza ni ile ya Mt.25:6 na Elia akatoka. Danieli pia aliisikia! Elia alipo isikia, akatoka kama vile inavyo andikwa katika Mt.25:6 lakini hakupewa kufahamu…
Sasa, ningependa nionyeshe hizo hatua tatu za shetani zitokazo shimoni. Kwanza upepo kubwa: ni vyama kubwa kubwa vya kiroho vinavyo zidi kutikisa dunia kwani hata Roho yenyewe yafika kama upepo kubwa. Matendo 2:2 inasema kwamba ikaja toka mbinguni kama ngurumo ya upepo kubwa. Na munaona ginsi gani hiyo upepo ya upako ilipasua na kutikisa milima ya siku hizi: marais wa nchi, mawaziri, matajiri, mamea, wana-bunge, wakuu wa inchi, wafanya biashara wakuu, wafalme, wakuu wa inchi, watu wenye sifa,… ndivyo ikavunja zaidi sana mioyo kuu za mawe. Munaona? Wote walichukuliwa katika hivyo vyama vya miujiza pasipo ujumbe. Wana wa ibilisi wanao vikwa upako wa shetani na watu hawa wanao jina la Yesu wametikisa mataifa, kuna mara wametambulika inchini mwao pasipo kujulikana duniani. Lakini Biblia inasema kwamba Mungu hakuwa katika ule upepo. Muliona katika makutano na makesha, watu wakianguka chini ya hiyo upepo ya upako. Kulikuweko hapa, katika Côte d'Ivoire, chama cha wa bulldozer wa injili,… hakuna mti uliyo weza kushindana nao! Kukawa aliko za mapepo ziitwazo maombi ya unabii au tangazo. Na katika 1 Wafalme 19, Elia alikuwa akiwasikia wakipazia Baali mungu wao sauti kubwa na kwa miungu, mapepo na sanamu za maji, za inchi, za mbinguni, za milima, za zahabu, za feza, za shaba, na za mawe ili hao wawarudishie baraka zao. Elia alikuwa akisikia: "Baali, rudisha malaika wangu! Mwamba, rudisha baraka zangu! Milima, munirudishie baraka zangu! Mbingu, mwezi, dunia, ninawanyanganya ndoa yangu, ninawaondosha kazi yangu, murudishe baraka zangu kwa jina la Baali! Ninaandika Baraka juu ya maisha yangu kwa damu ya ngombe [dume]! Ewe mume wa usiku, ninakokota sehemu zako za siri,… Nawe mke wa usiku, ninakata matiti yako,… Shetani, ninakutumia mashua kubwa kubwa za anga kwa vita, ninakutumia mabomu makubwa sana na sasa ninatuma bomu ya atomic katika kambi yako!!!...moshi inapanda toka kambi lako, ni mwisho wako!... Amina! Elia alisema: "je! Sikuwachinja wale kwa muto wa Kizoni? ". Na Elia alisema: "Nafsi zenu zipumzike kwa amani!" walipaza sauti nguvu zaidi. Walipiga mikono, walipiga miguu udongoni kwa jasho, walinyonga vidole na Elia alisikia: "ninavuta laana zangu na ninachovya kidole changu ndani ya damu ya ngombe na ninaandika baraka yangu juu ya dunia na juu ya mbingu. Nimebarikiwa na [sasa nina kazi kwa jina la Baali, mimi ni katika unyumba wangu pamoja na watoto wangu kwa jina la Yes… kwa jina la Baali ". Munaona? Ni uchawi. Katika Agano la kale na Agano jipya hakuna mahali hata moja,… Yesu na mitume wake hawakusema masemi ya dua! Ni uchawi. Vyumba vya wachawi; wachawi katika koti zilizo pakwa manukato. Munaona? Kulikuwa wakubwa na wadogo, wanaume na wanawake, maskini na matajiri walio jaa jasho, wakipiga miguu udongoni, wakipiga mikono, wakipaza sauti kwa jumla kwa nguvu kama iliyo mafundisho ya Baali; na Elia akakumbuka ginsi aliwaambia waseme kwa sauti kubwa. Tuisome: "Na ikawa ilipo timia saa sita Elia akawacheka, na akasema: museme kwa sauti kubwa, kwani ni mungu ; kwani anatafakari, au alikwenda mbali, au amesafiri ; kuna mara analala, hivyo ataamka! Na wakasema kwa sauti kubwa,…". Kiisha matangazo haya ya maombi ya dua, wakatwaa damu ya ngombe na… Biblia inasema katika 1 Wafalme 18:28 kwamba wakavuisha damu juu yao na Elia alisikia nje: "najichovia katika damu ya Yesu, ninatumia damu ya Yesu kama dawa, ninajiosha kwa damu ya ngombe, ninakunywa damu ya Yesu! Ninaweka damu juu ya mlango wangu, kitandani mwangu,… Dunia, ninaandika baraka yangu juu yako kwa damu ya ngombe, ninatangaza kusitawi kwangu chini ya damu ya ngombe, ninatabiri usitawi juu ya maisha yangu". Elia akasema: je! Sikuwachinja wale wote kwa muto wa Kizoni? Na Elia alisema : "Oh rehema! Nafsi zenu zipumzike kwa amani!" Nyakati moja moja, sauti moja ilikuwa ikipiga kelele kwa maneno kama haya: "tuliomba na tumejibiwa", na kundi ilikuwa ikijibu: "Kwa jina la Baali!... Kwa jina la Baali!,… Kwa jina la Baali!". Sauti ilisema na kundi lilijibu: "Kwa jina la Baali!!" kama ilivyo mafundisho ya Baali.
Karama kubwa kubwa za uchawi, utabiri, kunena kwa lugha, kupambanua, zilisibithisha ule uchawi. Kufikia mahali ambapo Biblia inasema kwamba ingewezekana, hata wateule wangelidanganywa. Ni nani angeliweza kutambua kwamba roho zinazo tenda ndani ya haya makanisa yote, misioni na huduma siyo Roho-Mtakatifu?...
Nyuma ya maneno haya, ilikuwa tetemeko la inchi. Wakati gani? Wakati dunia ilisulibisha ujumbe wa jioni. Pale, likawa patwa jua (mwezi) la tarehe 24 aprili 1993. Siyo tetemeko nyingi za inchi lakini tetemeko la inchi, baada ya haya ikawa giza. Kama anavyo sema Yoeli 1:4, wote ambao hawakudanganywa na upepo kubwa ilibidi wadanganywe na tetemeko la inchi. Ikiwa ujumbe wa jioni ni Yesu-Kristo, inabidi dunia ya kidini iusulibishe na ni kile ambacho wabranhamisti hawataki kukubali. Ujumbe uliyo letwa na Lutheri ulisulibishwa. Lakini walutheri hawataki kukubali. Ule uliyo letwa na Wesley, ulisulibishwa. Lakini wamethodisti hawataki kuikubali. Ila tu Wanakubali kusulibishwa kwa Yesu katika mwili, Yesu ambaye Yoane Mubatizaji alimwonyesha. Munaona?...
Tena, baada ya hii tetemeko la inchi, kukawa moto. Tuisome: "…Na nyuma ya tetemeko la inchi, moto: Bwana hakuweko katika moto ". Ile moto ilipashwa kuteketeza yote iliyo baki baada ya upepo kubwa na tetemeko la inchi. « …mabaki ya nzige, panzi akaila ; mabaki ya panzi funza akaila ; mabaki ya funza, ………..akaila». Yoeli 1:4. Na Yoeli 2:25 yasema kwamba ni Mungu mwenyewe aliye tuma [mambo haya]. 2 Thes.2:11-12 pia inaieleza. Munaona?
Hii hatua ya tatu ya shetani ikainuka toka shimoni na ilikuja… Wanamemba wa yale makanisa ndizo ngombe zilizo chinjwa na manabii wa Baali. Na Elia alisikia: "Moto!!! Moto!!! Moto!!!… Ninakuteketeza kwa moto! Moto wa roho-mtakatifu! Ninaalika moto! Moto!!! Moto!!! Moto!!!". Na mbele ya hii ushambulizi wa mapepo, palikuwa wasujaa wa imani. Wamoja ambao wamefanya siku makumi ine ya mafungo mara tatu au mara ine, wengine ambao wamekwisha kufanya siku makumi saba au hata siku mia moja ya mafungo, waGoliatha wa siku hizi. Wanefili wa nyakati za kale. Wa Goliatha wenyi miguu ya potopoto! Munaona? Siku makumi sita au siku mia moja ya kufunga chakula, ni kujipa malipizi. Munaona? Na kwa mbali, katika maono nilisikia: "Hu-ha! Hu-ha! Hu-ha!" na walikuwa wakipiga miguu udongoni. Munaona? Ilikuwa kama wanyama!
Elia alikuwa nabii wa moto. Karibuni alitoka kushusha moto katika 1 Wafalme 18:25-40 lakini hakujitambua katika vile vyama vya moto vilivyo kuwa nje. Tena Elia aliona kwamba kelele zilifanana tena zile za manabii wa Baali ambao alitoka kuwachinja. Kisha Mungu akamufunulia kwamba Roho yake itakapo tenda tena duniani, kwa mwisho wa nyakati, roho za manabii wa Baali ambao aliwachinja zitarudi tena duniani… Hao ambao ni Z. Tanee Fomum, D. K. Olukoya [msimamizi wa huduma ya mlima wa moto] walipita, makanisa za moto ya uwezo zilipita, vyama vya moto vilipita, misioni na huduma za moto walipita, wakipiga kelele kwa sauti kubwa: "Moto ya roho wa Baali! Moto ya roho-mtakatifu! Moto! Moto! Moto! Ninaalika moto! Moto!...". Ndugu, hao wanakwenda wapi? Biblia inasema kwamba wanakwenda pahali panapo itwa kwa kiebrania Armagedoni. [Kusanyiko linasema: Amina]. Ikiwa munaelewa semeni: Amina! [Kusanyiko linasema: Amina].
Biblia inasema kwamba manabii mia ine na hamsini wa Baali walialika moto juu ya ngombe na wakatabiri kwamba moto utashuka. Hawasemi tena moto ya Baali lakini [sasa wanasema] moto ya roho-mtakatifu. Japo ni zile zile roho za Baali. Sauti ya Kilio cha mateso ya manabii wa Baali ambao Elia alichinja inapanda toka hadeze hadi kutufikia. Elia alipo sikia pasipo kuchoka na kwa milele hata milele… "Moto! Ninaalika Moto! Moto! Moto! Moto! Moto inakuteketeza! Moto!...". Elia alisema moyoni mwake: "Nafsi zenu zipumzike kwa amani!" [Kusanyiko linasema: Amina]. Hawalazimishwe kuniamini lakini ni kweli mtupu. Wote wamewekwa roho ya Baali. Wengi hapa walifunguliwa toka mapepo wachafu je! Nilialika moto hata mara moja? Bwana aliwafukuza mapepo, aliwafungua watu mazimu, alifufua wafu lakini je! Muliona wapi akialika moto? Hata nyinyi wabranhamisti! Je! William Branham alialika moto hata mara moja katika maombi yake? Munaona? Moto ya Mungu ilipo shuka katika Mwanzo, iliteketeza Sodomo na Gomora. Elia alipo alika moto katika 2 Wafalme 1, ikateketeza hamsini za mfalme Ahazia. Katika 1 Wafalme 18, iliteketeza zabihu ya Elia. Munaona?
Mahubiri haya ni ufunuo kamilifu wa Yesu-Kristo. Sichoki kusema kwamba mtoto wa Mungu tayari ana mbegu ya Mungu ndani mwake. Wakati siku moja atasikia au kusoma ujumbe huu, atabariki Mungu na atasema: "Ni kweli! Ô! Nilianza kuona mambo yale! Nilianza kujiswali… Na nilipo anza kusoma ujumbe, kitu moja kama maganda ikaanguka toka roho yangu!!". Lakini mtoto wa shetani atakapo iona, atafazaika, hii si kwa ajili yake! Munaona? Atakwenda kuipatia mchungaji wake. Ndugu zangu! Shika mtoto wa Mungu, umufunge mikono na miguu na umupeleke mlangoni mwa kuzimu, atazunguuka chini na kwenda kuanguka katika paradiso. Shika mtoto wa shetani, umfunge mikono na miguu, na umpeleke mlangoni mwa paradiso na umueleze kwamba yuko mlangoni mwa paradiso lakini atakugeukia na kusema: "Basi mlango wa jehanamu ni wapi?"… Kwa sababu kilindi chake ni katika jehanamu! Wengi walikuja hapa pasipo kuhubiriwa lakini kwa ukurasa moja tu ya ujumbe huu ambao aliupata mahali fulani. Kwa upesi! Kwa sababu waliumbwa kwa Neno. Yote yatokana na kile tulicho toka mwanzo… mahali kote hii ujumbe utafika kutakuwa na uongofu. Mungu ataifanya kama inavyo andikwa katika Matendo 13:48! Kuhusu watoto wa shetani, hatuna uwezo wa kugeuza mapondo kuwa samaki wala ndege vikula maiti kuwa tai. Wao ni ndege vikula maiti wanao kusanyika kando ya maiti zinazo nuka, zinazo toa vidudu. Lakini sisi ni tai wanao kusanyika kando ya mwili ambao ungali moto ambao Tai kubwa wa Ufu.12:14 alituletea. Wana wa Mungu wanaamini kwa imani kwani ufunuo unakubalika kwa imani lakini wana wa ibilisi wanaukubali baada ya kuwaza na maswali mengi wakati akili yao inaelewa. [Kusanyiko linasema: Amina!]. Kama vile wayahudi, wana wa Mungu wanaamini kwa sababu nabii amesema! [Kusanyiko inasema: Amina!]…
Kunyakuliwa ni mlangoni. Mutazame tu kaskazini. Mungu atatumia kwa namna ya kimiujiza watu walio na elimu kamilifu ya uislamu ni hapo itakuwa mwisho. Mutakapo ona uislamu unatikiswa kwa uwezo huu duniani kote, hapo sasa ni pazia ya miaka karibuni 2000 ya mpango wa mataifa. Kama vile katika Mdo.3, hiyo uwingi wa viwete, vilema, na vipofu mbele ya moskiti wataponyeshwa na moskiti zitageuzwa kuwa hekalu. Ni hilo jambo moja tu ndilo linangojelewa na dunia ndipo kunyakuliwa kutafanyika. Ndipo hao maaskari warumi watasema juu yangu: "Hakika huyu Kacou Filipo alikuwa nabii wa kweli wa Mungu. Alituambia maneno haya!". Mt.27:54. Lakini makanisa watazidi [kutenda] wakiwa na huo huo upako ya uchawi kama vile hakuna jambo lililo tendeka. Watazidi kuhubiri… Ndugu zangu, kama Paulo, nimehubiri ufunuo wa Yesu-Kristo. Ni kwa ajili ya siri hizi ndipo nilipokea huo wito wa ajabu kwa mwaka 1993. Kama mtu akifikili kwamba mimi nina akili nyingi ndio maana ninafahamu mambo haya, ni shauri lake…
Kisha, ni sisi tutahukumu wale tulio wahubiri ujumbe huu. Makanisa nyingi zilizokuweko kabla ya garika zitakuja mbele ya Noa kwa kuhukumiwa. Na namna waliangamia katika garika, ndivyo watakwenda jehanamu. Wale walio mukata Isaya vipande vipande watashangaa kuona kwamba Isaya ndiye mwamuzi wao. Walio wachoma Yoane huss na Wycliff wanapo jidai kuwa upande wa Yesu watashangaa kuona kwamba wao ndio watawahukumu. Manabii na makuhani wa Yeremia 26:7-11 watakapo ulizwa mbele ya kiti cha hukumu, mbele yao watakuwa na yule walio mjua vizuri duniani : Yeremia, saratani iliyokuwa ikiwasumbua. Itakuwa ni kusaga meno…
Japo, Musa alipo rudi baada ya huduma yake, mlango ukafungwa. Ni nani basi aliye funga mlango ? Mungu peke! Siyo mjumbe anayefunga mlango lakini Mungu peke! Munaona ? Noa alipo ingia katika safina, Mungu akaleta muda mfupi ya neema kwa ulimwengu kabla yeye kufunga mlango. Mw.7 :16 inasema: « Na Bwana akafunga mlango juu ya Noa ». Munaona ? Musa alipo rudi nyumbani, Mungu akangojea siku chache kabla ya kufunga mlango juu ya Musa na kundi lake. Tangu Yosua, hakuna tena aliyeweza kuingia pamoja na Musa. Huu ni ufunuo wa upekee. Wote waliyo kuja baada ya hapo, Musa aliwaambia wakwende kununua mafuta kwa yule aliye kuwa akiuza mafuta baada ya kwenda kwake ndio kusema Yosua. Kila mara Mungu ana mtu moja aliye na funguo za ufalme duniani, mtu ambaye inabidi kumwamini kama inavyosemwa katika Yoane 6:28 inayo sema kwamba kazi na mapenzi ya Mungu, ni kumwamini yule aliye tumwa naye. Siku moja mubranhamisti mumoja aliniambia kwamba baada ya ndugu Branham kufariki, mwana wake Yosefu au Billy Paulo walikuwa wakifanya miujiza kama ile ya baba yao. Nilimuswali kama yale miujiza yanazidi hadi leo, akajibu: "Hapana!". Munaona ? yule mubranhamisti, hata Billy Paulo mwenyewe hawaelewi kwamba ni muda fupi ya neema iliyo pewa na Mungu… lakini mlango ulipo fungwa, mambo yale yote yakakoma. Hapo Yosefu Branham yeye mwenyewe hawezi kuokolewa katika kunyakuliwa ila tu akiwa na tumaini katika Kelele ya katikati ya usiku, anapo zidi kutenda kazi katika uwanja wa baba yake mpaka Kelele ya katikati ya usiku ya kweli itakapo kuja. [kusanyiko linasema: Amina]… kwa sababu tayari mlango umefungwa juu ya ndugu Branham. Na wakati Ewald Frank anapo eleza zoezi yake ya tarehe 3 januari 1981 juu ya kunyakuliwa, ninakubaliana naye wakati… aliona kundi la watu wasiyo weza kuhesabika waliyo vaa mavazi meupe, wakiwa katika hali yao ya ujana naye alikuwa kwa mstari wa kwanza. Lakini hasemi kwamba aliona ndugu Branham, au Paulo au Nevile. Ni kweli! Munaona? Aliona tu wale wanao mwamini.
Tena pale hukumuni, Paulo alikuja pamoja na kundi lake. Akajionyesha na kusema: "Bwana, uliniita katika ono na nilipokea kutoka kwako yale niliyo yahubiri… kama inavyo andikwa katika Wagalatia 1:11-12". Ikiwa Mungu hatamtambua Paulo halafu itakuwa ni mwisho kwa wale walio mfwata. Na wengi walikaribia, Martin Lutheri,… Kalvini,... John Wesley,… na hapo tunaona walutheri wakikuja. Wakasema: "Sisi pia tuliamini Lutheri, mtumishi wako mtakatifu!" lakini Lutheri akapaza sauti akasema: "Mimi!! Sikuwajua wakati wowote!! Muliniona wapi? Muliamini kwa mwaka gani?" wakajibu: "kwa mwaka 1560". Lutheri akasema: "Kwa mwaka 1560, ni Kalvini! Muwapeleke kwa Kalvini" [Amina!]. Lakini Kalvini akasema: "Bwana, walijidai kuwa watu wa Lutheri nilipo kuwa nikihubiri" na Kalvini akawapeleka kwa Lutheri ambaye hapo akawahukumu. Katika Luka 23:7 na 11, Pilato alipo tambua kwamba Yesu alikuwa wa utawala wa Herode akamurudisha kwa Herode. Nini basi itapitika hukumuni mwa kiti cha enzi cheupe? Kwanza wafarisayo walikuja, na kuliko wamuone Musa walimuona Yesu, walipatwa na woga na kusema: "sisi ni watu wa Musa!" Na Yesu akasema: "Kama ni hivi, muwapeleke kwa Musa ". Munaona? Musa aliwauliza: "je! Mulikuwa nami jangwani?… Wakati Koré pamoja na Dathan walijiinua, je! Ninyi mulikuwa kwa upande wangu? Je! Munawajua Haruni na Mariamu?" wakasema: "Hapana!" Musa alishangaa na kusema: "inawezekana mulikuwa nami Misri ila tu hamukutoka?" wakasema: "Hapana! Tuliishi duniani karibuni mwaka 30, 40! Lakini tulikuwa waaminifu kwako! «Musa alisema: "Kwa mwaka 30, pale ni Yesu! Lakini sasa, sababu gani basi munajidai kwamba nyinyi ni wangu? …Nendeni kwa Yesu!" [Kusanyiko linasema: Amina!]. Wakakumbuka kwamba Yesu aliwaambia katika Yoane 5:45: «Musizani kwamba ni mimi nitakaye wasitaki mbele ya Baba, kuna mmoja anaye wasitaki, Musa ambaye munamtumainia. [Kusanyiko linasema: Amina!]. Wesley angeweza kuwaambia walutheri walio kataa ujumbe wake: «Musifikirie kwamba ni mimi nitakaye wasitaki mbele ya Baba, kuna mmoja anaye wasitaki, Lutheri ambaye munamtumainia.» [kusanyiko linasema: Amina!]. William Branham angeweza kuwaambia wamethodisti: « Musizani kwamba ni mimi nitakaye wasitaki mbele ya Baba, kuna mmoja anaye wasitaki, Wesley ambaye munamtumainia». [Kusanyiko linasema: Amina!]. Nami nitaweza kuwaambia wabranhamisti: «Musizani kwamba ni mimi nitakaye wasitaki mbele ya Baba, kuna mmoja anaye wasitaki ninyi, William Branham ambaye munamtumainia. » [Kusanyiko linasema: Amina!]. Munaona? Hukumuni, wabranhamisti walio sikia na kukataa Kelele ya katikati ya usiku walikuja na ilikuwa tu hivi. Ni ya unabii! Ikiwa uliishi kwa mwaka 2002, wewe ni katika uongozi wa Mt.25:6. Hata wewe ni mkatolika, mprotestanti, wa kiinjili au mubranhamisti, fahamu kwamba ikiwa ni Mungu aliye nipa ujumbe huu… kama Isaya na Yeremia, yule aliye kuwa akiwahukumu ninyi duniani tangu 2002 atakuwa mwenye kuwahukumu mbele ya Mungu. Wafarisayo wanapo shika gombo ndefu wakijielekeza kwenyi kiti cha hukumu walisema: "Sisi ni wa Musa, … leo wangeweza kusema: Sisi ni wa Yesu!" [Makutano wanacheka] na hapo Musa akawahukumu kama vile imeandikwa katika Yoane 5:45! Unapo tupilia mbali ujumbe wa wakati wako, mafungo na maombi yako ni machukizo mbele ya Mungu. Zaka na sadaka zako ni machukizo mbele ya Mungu. Bidii yako, matunda yako ya Wagalatia 5:22 ni machukizo mbele ya Mungu, hasa zaidi ya yote, Yesu wako ni shetani.
Ndugu [zangu], nimekuwa haraka kusimama pamoja na makanisa haya mbele ya Mungu. Ikiwa hata yule aliye mnyenyekevu zaidi, mtakatifu zaidi au wa kiroho zaidi kati yao atakwenda mbinguni hapo Mungu hakusema nami. Kama vile kwa wakati wa Noa, yule Mungu ambaye wanajidai kumwabudu atawaangamiza wote. Wao na wachungaji wao, waakilishi wao, manabii wa Baali na umati wa roho takatifu wao…
[Kusanyiko wanaimba: Ni siku gani Bwana, Neno hili litajifanya mwili ndani mwangu? Kama vile wimbo huu, nyimbo zimewekwa kwa utaratibu wa ujumbe huu zikishughulikiwa na waimbaji].
kurudi kwa utaratibu