MAHUBIRI N°4

MAFASIRIO YA UFUNUO 2, 3, 6, 13 NA 17

(Ilihubiriwa Jumapili 20 oktoba 2002 huko Locodjro, Abidjan – Côte d’Ivoire)



     […] Inafaa kuonyesha hapa kwamba, kama mihuri saba na zambi ya asili, Mungu alitujulisha nyakati saba kwa hhuduma ya William Branham kwa wakati wa jioni.

    Tangu Roho Mtakatifu ilishuka katika Matendo 2 mpaka kunyakuliwa, Kanisa la mataifa liligawanywa kwa wakati au nyakati saba. Kwa wakati Fulani, Kanisa itafanana kusanyiko Fulani. Sasa:

    Ufunuo 2:1-7: Wakati wa Efeaso (ku anza 53 mpaka mwaka 170), mjumbe wa wakati huu ni mtume Paulo. Kanisa inasumbuliwa na watumishi wa Mungu wa uongo (2 Petro 2; Yuda). Mafundisho ya uongo yanaanza, wanikolai, mtu anataka nafasi ya Mungu. Nyama inayotoka ni Simba (Ufu.4:7), Neno.

    Ufunuo 2:8-11: Wakati wa Smirna (tangu 170 mpaka 312), mjumbe wa wakati huu ni Ireneo. Mungu alipandisha wajumbe wengi nyuma yake lakini yeye ndiye baba wa wakati huu: Roma ya kipagani inatesa Kanisa. Wakristo wananyanganywa vitu vyao kwa ajili ya imani yao. Wanawaomba kutoa sadaka kwa sanamu  ili wasiuawe. Ndama inatokea kwa toleo.

    Ufunuo 2:12-17: Wakati wa Pergamo (tangu 312 mpaka 606), mjumbe wa wakati huu ni mtakatifu Martin. Mwanzo wa kanisa katolika. Ubalama ni kupenda pesa, anasa, na kuabudu sanamu. Kwa wale wanao penda kuhesabu wajumbe wa Mungu duniani, Biblia inasema wazi kwamba katika wakati huu, Mungu atatumia mtu aliye mwaminifu kwake, na kwamba huyu mtu atawekwa mautini kama Antipasi. Na hata, mtu ambaye kupitiya yeye tulijua vitabu 66 vya Biblia haitwi kwa jina la Paulo, Wesley, Lutheri au Branham lakini Uzebi, na ni kwa nguvu ya utume wa umungu ndipo mtu anaweza kufanya ile kwa ulimwengu.

    Ufunuo 2:18-29: Wakati wa Thyatiro (Tangu 606 mpaka 1520), mjumbe wa wakati huu ni Kolomba. Mungu anahamakia Kanisa kuiacha kanisa katolika iwadanganye watu kama leo wanaangalia makanisa za kiinjili na za kiprotestanti zinapodanganya. Muda wa miaka 914, walifwatana wajumbe wasujaa wa Mungu mwingine baada ya mwingine.

    Ufunuo 3:1-6: Wakati wa Sardi (Tangu 1520 mpaka 1750), mjumbe wa wakati huu ni Martin Lutheri. Nyama wa tatu anatoka, ni wakati wa Martin Lutheri juu ya kuhesabiwa haki kwa imani, na wa Yoane Kalvini juu ya kutangulizwa mara mbili.

    Ufunuo 3:7-13: Wakati wa Filadelfia (Tangu 1750 mpaka 1906), baba wa wakati huu ni John Wesley. Ni mwanzo wa zihirisho za kiroho. Ni wakati wa John Wesley na Georges Whitefield. Hawa wawili walitengana juu ya kutangulizwa.

    Ufunuo 3:14-22: Wakati wa Laodikia (Tangu 1906 mpaka…), baba wa Nyakati hii, ni ndugu Branham na hii wakati itafikia mwisho kiisha mateso ya mabikira wapumbavu. Tai (Ufunuo 6:7), Roho ya unabii na ya neno. Pia roho ya nyoka inajifunua kama nabii katika makanisa.

    ANGALISHO: Wanyama nne ni kujitambulisha kwa ileile Roho [ya upekee] ya Mungu katika Nyakati. Wanachunga Kanisa iliyo hai (Ezekieli 1:4-12). Wao ni injili nne zinazo linda kitabu cha matendo ya mitume au makerubi wanaolinda mti wa uzima (Mwanzo 3:24)  au pia kabila kumi na mbili, tatu kwa kila upande, wakichunga sanduku ya agano.     

      MIHURI SABA ZA UFUNUO 6 NA 8:1                                                                       

      Muhuri wa kwanza: Ni simba anayeita Yoane aje atazame. Kama Danieli, (Danieli 12:4) Ngurumo, sauti ya Mungu (Kutoka19:16/ Yoane 12:28-29) zilimtafsiria mambo haya lakini alikatazwa kuyaandika mpaka wakati wa  mwisho (Ufu.10:4). Ngurumo saba hapa ni sauti ya Mungu ikifasiriya mihuri saba kwa wakati wa kurudishiwa kwa kila kitu (Laodikia). Mpanda farasi anasonga mbele na upinde lakini bila mishale. Anaogopesha tu lakini hawezi kufanya kitu. Kwanza hana taji kwani ni roho, [ni] mafundisho tu (Ufu.2:6): unikolai. Lakini alipokea taji alipofanyika papa, mpinga Kristu. Ni kwamba kila prezidenti wa kanisa ni mpinga Kristu.

     Muhuri wa pili: Nyama nne za Yoeli 1:4 na 2:25 na wapanda farasi nne wa Ufunuo 6 ni kitu moja. Ni uleule mpanda farasi anayebadilisha farasi, hhuduma  au hali. Ile kanisa ilikuwa nyeupe kama Kanisa ya kweli lakini alipoanza kuwauwa watakatifu… rangi nyekundu ni damu ya mitume, waprotestanti, wakristo milioni 68 waliuawa kwa kanisa katolika ya Roma. Na papa akijiita msimamizi mwaminifu wa Mungu duniani, mpatanishi mkuu kati ya Mungu na watu, baba wa mitume. Majina ya makufuru (Ufunuo 13:1). Yeye ni msimamizi wa dunia, mbinguni, na wa utakaso wa roho kisha kufa.

     Muhuri wa tatu: ni wakati wa uchuruzi. Inafaa kutoa zahabu na feza kwa kuingia katika Paradiso. Inafaa kulipa ili usamehewe zambi. Mzabibu na ngano = uzima. Mafuta = Roho, lakini Mungu anamkataza kuwatendea mabaya wachaguliwa, kuwasukuma kusema kwa ufahamu “nakuamkia Maria” au kuomba wafu au kutoa sadaka kwa sanamu za kuchonga. Lutheri alitoka na ujumbe: “mwenyi haki ataishi kwa imani”

     Muhuri wa ine: Wakati wa Laodikia unaanza, ni tai anayetoka kwa kupiganisha roho ya uchawi. Rangi kama nyeupe ni mchango wa makanisa pamoja na uwezo wa siasa, wa kidini na wa uchumi. Mkusanyo wa vipindi hivi vitatu. Taji tatu katika moja, rangi tatu katika moja, utatu wa rangi, farasi, huduma: mpinga Kristo, nabii wa uongo na mnyama. 

    Muhuri wa tano: kwa kila muhuri, ni ngurumo saba zinazo tafsiri siri zilizo ndani. Kwa mfano, kwa mtoto;  W, D, å, na Y ni vitu vilivyo tiwa muhuri (vinafichwa). Lakini sauti inayosoma au “kutafsiri” hizo herufi nne ni ngurumo saba. Ngurumo ni sauti ya Mungu. Yne.12:28-29 inasema: “…sauti ikatoka mbinguni: nimelitukuza na nitalitukuza tena. Basi makutano waliosimama karibu wakasikia, wakasema ya kwamba kulikuwa ngurumo; wengine wakasema malaika amesema naye. Unaona? Na Kut.19:16-17 pia inaieleza. Watu wanasikia ngurumo lakini nabii anasikia maneno. Ufu.10:4 inasema nini: “hata ngurumo saba zilipotoa sauti yao, nilikuwa tayari kuandika; nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema: tiya muhuri juu ya maneno zilizosema ngurumo saba, usiyaandike”. Munaona? Ngurumo ni sauti ya Mungu.

     Basi wakati muhuri wa kwanza ulivunjwa, ngurumo saba zikafunua yaliyomo. Muhuri wa pili ulipovunjwa, ngurumo saba zikafasiria mifano zilizo katika hiyo muhuri. Vilevile mpaka muhuri wa sita. Nafsi zilizo chini ya mazabahu ni wayahudi waliyouawa huko Ujermani, Italia, Ufaransa, URSS. Wanajua tu sheria ndio maana wanaomba haki kuliko kusamehe. Sheria: jicho kwa jicho, jino kwa jino. Hapo hawakuokolewa kama wayahudi lakini kama wachaguliwa wa mataifa.

     Muhuri wa sita: mbingu kutiwa giza inaonyesha umuhimu wa ukombozi wa wayahudi sawa kwa Misri hiyo muhuri inapitika katika Ufu.11 pamoja na Eliya na Musa ambao ni taa mbili. Mat.24:4-5 (muhuri wa 1), Mat.24:6 (muhuri wa 2), Mat.24:7 (muhuri wa 3), Mat.24:9-13 (muhuri wa 4 na wa 5), Mat.24:29:30 (muhuri wa 6), Mat.24:36 (muhuri wa 7).

    Muhuri wa saba: Kwa Mat.24:36 na Ufu.8:1, tunafahamu kwamba muhuri wa saba ulipo vunjwa, ngurumo saba zilinyamaza. Kwani ina siri ambazo siku zake za kutimizwa hazinge paswa kujulikana. Ni katika hiyo muhuri kulikuwa lugha isiyojulikana. Ilifunguliwa kwa wakati wa mangaribi lakini ufunuo wake iliweza kumalizika pamoja na ujumbe wa wakati ambayo ni tu tafsiri ya lugha isiyojulikana iliyoachwa pembeni. Na mjumbe wa wakati wa jioni alisema kwamba ni nyuma ya hiyo lugha isiyojulikana ndipo mvuto wa tatu (3ème Pull) inapatikana.  

     Bahari au maji maana yake ni watu, mataifa, lugha na makabila kufuatana na Ufu.17:15. Mnyama aliye na vichwa saba na pembe kumi ni utawala wa Roma ambao ni nyama wa nne wa Danieli 7:2-12, ndio maana inapatikana kwake nyayo za zile nyama zingine tatu alizozimeza. Danieli 7:4 ni utawala wa Babiloni iliyo Simba, shahiri la 5 ni utawala wa Medi na Persi ambayo ni dubu, shahiri la 6 ni utawala ulimwenguni wa ugiriki ambayo ni chui, pembe kumi ni falme kumi au mataifa kumi. Kwa Ufu.13:3 ni ukristo uliyotaka kumaliza [ule nyama] lakini yeye pia akajifanya wa kidini na akashika tena dunia.  Utawala wa kipagani ikageuka kanisa moja duniani kote na ikamupa mamlaka mtu mmoja aliye na majina ya makufuru: “msimamizi wa mwana wa Mungu Duniani [vikariv’s filii dei], papa mkuu, mtangulizi wa Yesu-Kristo, baba wa ulimwengu wote, akida wa mitume, aliye kuja nyuma ya Petro, akijifanya asiyeweza kuanguka kama Mungu. Majina hizo pia ni makufuru  kama vile: mumethodisti, mubatisti, mupentekoste,… 

     Katika Ufu.13, mnyama wa shairi la 11, anapanda juu toka dunia, inchi moja inayotawala dunia sawa Roma na ni Marekani (USA). Pembe zake mbili ni mamlaka ya siasa, uchumi na mamlaka ya kidini. Kama mwana kondoo, nchi hiyo ni ya kidini, inaapa juu ya Biblia lakini inajiweka [kwa kutawala] kama joka ikitumia shurti hapo, ikiweka sheria ya kufungia [nchi Fulani] pale, inapo ripua pasipo ukubali wa UMOJA WA MATAIFA. Inashusha moto toka mbinguni: miripuko tangu Hiroshima na Nagasaki. Ni kwake ilitokea sanamu ya kanisa katolika ni kusema makanisa za kiprotestanti na za kiinjili. Chapa ni roho. Juu ya kipaji cha uso ni: kukubali, juu ya mkono wa kuume, ni kutumika katika makanisa hizo. Shairi la 17: yule asiyeweza kutumika katika roho moja na MAREKANI (USA), anakuwa jambo la shurti au kumfungia kama “Cuba”, Libia, hawezi kununua kitu wala kuuza kutoka nchi nyingine. Hiyo roho ya shurti na kufungia ilianza zamani na zile utawala za kwanza. Biblia inaizungumzia katika 2 wafalme 6:24-25. Na sasa, hiyo kufungia [nchi Fulani] inaleta njaa kwani hauwezi kununua wala kuuza. Tuisome: « Na ilikuwa nyuma ya maneno haya, Beni-Hadadi mfalme wa Suria, akakusanya majeshi yake yote, akapanda, na kuizungusha Samaria kwa vita. Njaa ilikuwa kubwa kule Samaria na tazama, wakauzunguuka kwa vita, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande makumi nane vya feza, na kipimo cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya feza. ». Na 2 wafalme 17:4-5 inasema kwamba utawala wa Asuria, uliyoitawala dunia nzima kwa wakati ule, ikaweka shauri ya kufungia Samaria kwa miaka mitatu. Tusome shairi la 5: "Na mfalme wa Asuria akapanda juu ya nchi yote, akakwenda Samaria, akauzunguka kwa vita miaka mitatu". Tunaiona tena katika 2 wafalme 25:1-7, shauri ya kufungia ya Babiloni juu ya Yerusalema. Hakuna aliyeweza kununua wala kuuza na shairi la 3 linasema hivi: «Siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ilikuwa nzito ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu. ». Na hiyo roho ilitumika kwa utawala wa Roma mpaka kuharibu Yerusalema kwa mwaka 70 kisha ile roho ilitenda kwa kanisa katolika ya Roma na sasa inatenda kupitia Marekani. Kwanza walisema kwamba ni kuzunguuka [nchi] nyuma walisema ni pigo na sasa wanasema ni kufungiwa. Kwa mfano: mwaka 1400, papa Yoane XXII akatia Ujermani kwa pigo kwa sababu ya kukataa kunyenyekea na mwenendo mbaya ya Louis IV wa Bavière kuhusu papa. Na kwa mwaka 1347, Louis IV wa Bavière akakubali kwa sababu Ujermani ilifanywa zaifu kwa miaka 25 ya pigo, kwa maana hakuweza kununua wala kuuza. 

      Na hiyo roho itatumika [tena] katika makanisa maana kwa kufaidika na wema ya wakubwa wa nchi au duniani kote, inafaa kuwa mwanamemba wa shirikisho la makanisa au wa shauri la taifa au ya dunia nzima kwa makanisa za kiprotestanti na za kiinjili. Kufuatana na shairi la 8, tunaona kwamba ni "wale majina yao hayakuandikwa tangu kuwekwa misingi dunia katika kitabu cha mwana kondoo " ndiyo wale watabaki mpaka mwisho katika makanisa hizo za kikatolika, za kiprotestanti, za kiinjili, za kimisioni na huduma pia katika zile zote za kibranhamisti. Kwa shairi la 10 imesemwa: "kama mtu akichukuwa katika kifungo…" wabatisti, wabranhamisti na wengine wanao tangaza injili. Inje ya ile ambayo Mungu iko akifanya, ingine yote inachukuwa katika kifungo. Wakati Tunapokuwa tukitaka kuwaokoa watu kutoka hivi vifungo vya kidini, wengine wanatafuta kuwapeleka kule. Kwa wakati tuko tukichoma biblia Tob na Louis Segond, [wao] wanazigawanya. Munaona?

    Zaidi, katika musemwa ya unabii, mwanamke ni mfano wa kanisa moja. Katika Ufunuo 17:1, huyo mwanamke ni kahaba, alipokea mbegu kutoka masuria wengi. Biblia inasema kwa shairi la 15 kwamba ameshimikwa pahali pote katika mataifa, lugha, watu, vijiji, makambi, Ma Rais na Wafalme, maliwali na maakida wanafanya urafiki na kanisa hiyo. Amekaa juu ya milima saba: Capitol, Palentin, Caelius, Esquilin, Aventin, Quirinal na Viminal, mashairi 9 na 12. Shahiri la 4 inafunua utajiri wake. Shahiri la 5 linasema kwamba yeye ni mama wa wingi wa makanisa kahaba: kanisa la kiluteri, kanisa la Zwingli, kanisa la kikalvinisti, kanisa la kipresbiteri pamoja na John Knox, kanisa la kianglikani ambayo ilijulikana na kukubaliwa katika Uingereza kwa mwaka 1500 kisha Henri VIII kujitenga na Roma, namna moja ya kutosikilizana kwa ukatolika na ukalvinisti. Nyuma ya hayo wa “puritains” kiisha kanisa la wamethodisti kwa wakati wa uamsho wa Morave, kiisha kwa ngambo moja, kanisa la kristo pamoja na  Alexandre Campbell, kanisa la ubatisti pamoja na John Smith aliyetupilia mbali ubatizo wa watoto wadogo na kumwangiwa maji,… kwa ngambo ingine, katika makanisa za kimetodisti kukatokea kanisa la kinazareti kiisha kanisa la wa “pelerins” wa utakatifu, kiisha kanisa la wapentekoste kiisha kanisa la kusanyiko za miungu ambayo ni tawi ya mgawanyiko uliyo fanyika kati ya wapentekoste kwa mwaka 1906. Ilikuwa kwanza jina la “shauri kwa jumla” nyuma [ikawa] “kusanyiko la miungu. Kila moja ya makanisa hizo ilitoa uwingi wa matawi kama inavyoonekana leo kwa wabranhamisti.

      John Smith alikuwa mwenyi kupenda kusanyiko, alitoka kwa kanisa la anglikani na akajibatiza mwenyewe kwa kujimwangia maji kichwani. Yeye ni baba wa makanisa zote za ubatisti.

      Hakuamini kwamba kuna zambi ya asili na akasema kwamba watoto hawana zambi. Lakini wakati John Smith alikufa, ni mfwasi wake Thomasi Helwys ndiye aliunda kanisa la kwanza la ubatisti. Simusahau Menno Simons, huyu padre mzee wa katolika ambaye ni muundaji wa oroda ya wa “Mennonites” na alirudisha kanisa lisilo la ubatisti. Munapaswa kujua mambo haya yote mbele ya kujiunga na kanisa Fulani. Wakati mwanzo wa kanisa ni mbaya au mwanzilishi ni wa uongo, haizuru mambo gani utafanya ndani yake, ni bure, utakwenda tu katika gehena. Ni kama huyo mwanamke mchawi kwa jina la Aimée Semple Mcpherson aliye unda kanisa “foursquare” kwa mwaka 1922, mu canadia aliyekuja kukaa huko Los Angeles.

      Vema! Roho ya uchawi inawaambia watu kwamba mwanamke na maji ni “bibi wa maji”. Ni kuzubaisha kwa Shetani. Kitabu moja ambacho kinazungumzia “bibi wa maji” ni kitabu cha Enoka katika sura yake ya 9 kwa shairi la 2. Lakini kitabu hiki hakikukubaliwa katika “canon” ya wayahudi; ni kusema ni kitabu cha ibilisi. Kahaba ni mwanamke asiye na mume moja, lakini [ana] masuria. Makanisa hizo hawana mchungaji wala kuhani mmoja. Moja anakuja na anakwenda zake. Mwingine anakuja, anakwenda zake. Na mtoto haramu anakamata jina la mama wake: “mimi ni mkatolika, mbatisti, ndugu wa ujumbe (branhamisti). Shairi la 6: alilewa kwa damu ya watakatifu, ma milioni za wakristo waliyo uawa ndipo Yoane alishagaa kuona kwamba kulikuwa kanisa ambalo liliweza kufanya mambo yale. Shairi la 8 linaonyesha kwamba makanisa zile zinapanda kutoka shimo, kwa roho watakatifu wao wanaopanda kutoka mitoni na maji na kilindi cha bahari kwa kuenda jehanamu na mauti na hadeze* zinafwatana nao. Wakiwa katika mito hizo, maji na vingine, walikinga makabila, watu, vijiji, jamaa. Hiyo ni nini? Walikuwa makerubi walinzi waliyo poromoshwa zamani kutoka mbingu. Na sasa wanakuwa walewale makerubi walinzi kwa jina la Yesu Kristo. Kila kanisa, misioni, na huduma inakuwa na kerubi moja kwa kichwa chake: maprezidenti wa makanisa, wa Osborn, Benny Hinn, Yonggi Cho,… na wote wanaohubiri chini ya huduma yao ni malaika ambao mkia yao iliokota katika vita kubwa pamoja na malaika mkuu Mikaeli kufuatana na Ufu.12, malaika waliyo danganywa mbinguni.

      Vema, shairi la 16 linasema nini: « Na pembe kumi ulizoona na nyama, hao watachukia Yule kahaba na watamfanya kuwa tupu na uchi na watakula nyama yake, na watamteketeza kabisa kwa moto…». Na kwa hizo falme kumi ambazo ni… Uingereza, Portugal, Ufaransa, Ujerumani, Spanish, Autriche, Italia, Pologne, Rusia, na nyingine kulisimama wanyama wa kiroho ambao ni kanisa ya kiluteri, kanisa la kinazareti, kanisa la kibatisti, kanisa la methodisti, kanisa la kikalvinisti, na kanisa presbyterienne ambao walifanya tupu kanisa katoliki wakichukuwa wanamemba wake na wakamwacha bila kitu. Walikula mwili wa kanisa katolika. Munaona? Na sasa pembe kumi ni kundi ya makanisa za kiinjili na za wa branhamisti.

      Turudi kwa shairi la 10, Yule aliye ni Kaisari, anaye kuja ni Nero aliyetawala miezi sita ya ukali. Wanaopatikana katika makanisa hayo watashangaa lakini sisi tunajua kwamba watakwenda katika gehena. Wa 8 ni mfululizo wa wapapa. Shairi la 12: ni waprezidenti pasipo taji: Hitler, Staline, Mussolini … wana mpango moja na kanisa katolika; moja aliua wakristo, wengine waliua wayahudi. Mji ni Vatikani.


Tuma ukurasa huu kwa rafiki

kurudi kwa utaratibu

www.matth25v6.org - Copyright © Aprili 2007
Kisheria Deposit ® All rights reserved