[Usomi wa mahubiri: 2 Wafalme 5:1-27] Mara kwa mara ninasikia ikisemeka kwamba viongozi na wakuu wa siasa kwa siri wanaita manabii, wachungaji na wasimamizi wa makanisa na hao wanawawekea mikono ili wawekwe kwa kazi katika wizara au wasiondoshwe kazini au kwa kukubaliwa wala kupata neema machoni mwa rais wa jamuhuri, waziri na kazalika. Ikiwa biashara yako haiendeki, kama unashindwa maishani, ukipenda kupandishwa cheo kazini mwako, kuhusu ndoa, ukipenda kuingia katika nyumba mpya au kuiondoa ulozi,… kama wewe ni mkristo au hapana, uwakwendee manabii na wachungaji wa siku hizi na hao watakufanyia utakacho! Maana yake ni nini? Biblia inasema katika Ufu.12:7-9 pia katika Isaya 14 kwamba kulikuwa vita mbinguni kwani Shetani alipenda aabudiwe kama Mungu. Shetani alisema: "Nitapandisha kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu na nitakaa juu ya mlima wa agizo… nitafanana na Mjuu-Sana...". Malaika wa Mungu basi wakapigana na Shetani na malaika wake na kuwatupa duniani. Ma mia za kundi za wamalaika wakatupwa duniani na hao wakakwenda kujificha nyuma ya maji, nyota, pori, na mwitu takatifu, karamu, orodha za uchawi katika inchi zote. Kuliko kuitwa "pepo wachafu" au "malaika walio anguka", katika Afrika waliitwa: malaika watenda mema. Na hao malaika wakapandisha wachawi wakuu. Waliabudiwa na hapo wakafikia nia yao ya kwanza. Waliyo kuwa wakuu kati yao walikuwa kabisa miungu, kama vile huko Misri, kwa wa Inca, huko Babiloni, huko India na penginepo. Kama inavyo andikwa katita Ufu.14:6-8, Injili iliamuru ulimwengu kujitenga na haya mapepo. Kwa mara ya kwanza ikajulikana kwamba mfumu, mchawi, majusi ni nabii wa Shetani. Mbalimbali na wafalme, ilikuwa wachawi na waganga wa kienyeji ndio walikuwa wakiishi maisha ya raha: mbuzi nyeusi, kondoo, kuku nyeupe, chupa za pombe kali… viongozi na wakuu wa siasa wanawaita kwa siri kusudi wapewe kazi katika wizara na kazalika au ili wabaki katika hizo kazi. Ikiwa biashara yako haiendeki, ikiwa unashindwa katika ndoa yako, kazi yako, shuleni, kusudi upandishwe cheo kazini, nyumba yako inasumbuliwa na mapepo au imelogwa… uwakwendee hao wachawi, wafumu, waganga wa kienyeji! Na sasa angalieni namna gani hao manabii wanaishi katika raha! Wao ni wachawi ambao tu wamegeuza sura, wote kabisa. Mazabahu na mahali pa juu sana katika 2 Wafalme 17:29-31, hiyo hiyo mazabahu ya 1 Wafalme 11:5-7 zimegeuka kuwa makanisa, misioni na huduma kwa leo. Na wakati serikali inapo leta kibali kwa moja ya haya makanisa, misioni na huduma, ni uchawi ambao unawekwa kisheria. Na sasa munasikia katika makutano yao: "Kwa msaada wa Bwana Yesu-Kristo na katika wepo kamilifu wa Roho-Mtakatifu,…". Munaona? Na niliambiwa kwamba kuna mahali ambapo wametayarisha kiti cha heshima na kitambaa kyeupe juu yake. Ninyi wafumu wa siku hizi, mukumbuke kwamba, hizo mapepo munazoita Yesu-Kristo au Roho-Mtakatifu zilipo kuwa porini, mababu wenu walitenda kama ninyi, wakitayarisha viti na vitambaa juu yake. Inabidi musisahau…
Vema, tusome sasa 2 Wafalme 5 [Ndl: Ndugu Filipo anasoma sura 5 yote.]… Vema! Kupitia msichana mdogo, waziri wa jeshi la Suria akakwenda Israeli kukutana na nabii Elisa, ambaye peke yake alikuwa nabii wa kweli kwa wakati wake, kusudi apokee uponyaji wa ukoma wake. Kwanza waziri Naamani akamwendea mfalme wa Israeli ili akaribishwe wazi wazi kwa heshima ya kiaskari hata vituo vya upashaji wa habari viweze kutangaza mambo yale. Wakaifanya iwe jambo la kujulikana! Tena angalieni shairi la 9, waziri Naamani anapo jielekeza kwenyi nyumba ndogo la nabii Elisa pamoja na magari za vita, farasi, wasujaa wa jeshi, batalioni zenyi kukingwa, kikundi cha wapanda farasi wenyi kukingwa. Yote ile ni kwa kumwonyesha nabii Elisa kwamba yule anaye kuja siyo mtu bure. Watu walitoka pembeni ya barabara kwa kutazama umati wa watu ambao walikuwa njiani pamoja na filimbi na kundi la wapanda pikipiki… Bila kuhesabu hotuba ambayo ilimubidi atamke, akileta maelezo juu ya vipande elfu sita vya zahabu na milioni kumi ya feza kama alivyo zoea kufanya katika makanisa mengine akishangiliwa. Kwa mbali, filimbi zilisikika, kisha wanao tembeza pikipiki wakaonekana, hapo waziri Naamani na jeshi lake lote hawakuwa tena mbali… Wakaja na kusimama nje wakingojea heshima kutoka kwa Elisa lakini hapo walidanganyika kwa huyu nabii. Munaona? Naamani alipo fika mbele ya makao ya Elisa, akasema moyoni mwake : "je! Mapambo ni wapi kuhusu ujio wangu? Labda siyo hapa?". Hakika ilikuwa ni pale! [Kusanyiko linasema: Amina!"]. Munaona? Elisa aliona nje maskini msuria aliye pofushwa kwa utajiri na sifa za dunia hii na ambaye mateso ya jehanamu ilimngojea ikiwa hangeli weza kutubu. Elisa aliona ukoma wa mwili wake, wa nafsi yake, wa roho yake na hapo tibabu ilikuwa ni zoezi la Yorodani. Nyuma ya hii vazi la kijeshi au koti Elisa alisikia arufu ya uharibifu. Ni vile! Naamani alitamani pia heshima kutoka kwa huyo nabii wa upweke lakini, Elisa akatuma mjumbe amwambie: "Kwenda na ujitupe mara saba katika Yorodani na utakuwa safi." Akapata hasira! Alianza kufahamu kwamba yeye Naamani, mtumishi mkuu wa Suria ndogo hakuwa kitu mbele ya mtumishi mdogo wa Mungu mkuu. "Namna gani anaweza kuniambia nikwende kujitupa ndani ya maji ya potopoto kama Yorodani! Parpar na Abana, mito za huko Suria si nzuri zaidi? Alisema: "Je! Ilikuwa lazima yeye anibatize?… hata nabii yeye mwenyewe hakuji na sasa anatuma tu mtu mdogo?" watumishi wake walisema: "Mwalimu, kubali!…" Alisema: hatukutayarisha vazi kwa ubatizo! Watumishi wake wakarejea: "Mwalimu, kubali!…" Munaona? Alihitaji uponyaji, lakini alitamani uponyaji kwa heshima kuu. Naamani hakuwa hata tayari kupiga magoti kwani nguo yake itaweza kuchafuka magotini. Alisema ndani mwake: Je! Ilikuwa lazima nifanye hivi? Je! Ilikuwa lazima mimi nifanye vile? Watumishi wake walisema: "Bwana, kama nabii angelikuomba jambo kubwa, je! Hungeliweza kulifanya? Sasa yeye amekuambia tu: Ujioshe na utakuwa safi! Bwana, kubali!...". Angalieni shairi la 11: « Na Naamani akakasirika, na akakwenda zake, na akasema: Tazama, nilisema ndani mwangu: hakika atatoka, na kusimama pale, na ataita jina la Bwana, Mungu wake, na atatembeza mkono wake juu ya ugonjwa na hivyo atamwokoa mkoma » Munaona? Njiani, tayari Naamani alikuwa ameweka mpango wa kupokelewa kwake na ya uponyaji wake. Lakini… Alipo kuwa bado angali Suria, kama angeli jua kwamba yeye Naamani ataweza kutendewa kama mtu wa kawaida, hangeliweza kuja. Oh! Maskini Naamani! Lakini kwa mwisho, akajitupa mara saba katika Yorodani na ukoma ukamwacha na akawa safi. Akarudi kwa Elisa ambaye huyo akamuhubiri Kelele ya Katikati ya usiku ndipo baadae, akamwambia Elisa kwamba hawezi tena kutolea zabihu kwa miungu wengine, hata katika kanisa moja. Alibadilika, hakufurahia tena maongezi ya kukaribishwa, kiti cha mapokezi kwani alifanya zoezi la Yorodani… Oh! Zoezi la Yorodani!
Kwa shairi la 9, Naamani alitaka kusimama mbele ya mazabahu ili atamke mambo mazuri ambamo ndani mwake atoe maelezo juu ya vipande elfu sita vya zahabu na milioni kumi za feza na pia nia yake ya kuweka lami katika kijiji cha Elisa, na kutuma humo umeme, maji safi na hospitali ya umama. Ijapo hali iliyo julikana, angeli onyesha uhusiano bora ulio kati ya Israeli na Suria. Munaona? Angeli weza kusema: "… mimi, Naamani mnyenyekevu, waziri wa jeshi la Suria, nimepokea mara tatu cheti cha heshima… nina cheti cha orodha ya kustahili cha inchi fulani na inchi fulani!...". Munaona? Alikosewa tu kitu kimoja: Zoezi la Yorodani. Alitamani kujulikana na ukuu wa ubinadamu, hapana wokovu! Ukoma wa kweli wa huyo waziri, ilikuwa ni hizo peta zake za kiaskari, utajiri wake, gari zake na nyumba yake ya anasa ambavyo vilimupa kufikiri kwamba yeye ni mtu mkuu. Munaona? Naamani alisema kwa shairi la 11 kwamba alizani nabii atakuja yeye mwenyewe na kumuomba wala mafungo ngumu ya siku tatu au sadaka kubwa. Ndio maana alitayarisha milioni sita, alijua kwamba manabii wanapenda feza. Manabii wa makanisa za Parpar na Abana. Lakini kisha zoezi la Yorodani, alisema: " Sitakwenda tena kutoa msaada wangu au kushikilia haizuru nini, hata kama itanibidi kuachishwa cheo changu cha uwaziri, mwana-bunge, mea,… sitakwenda tena kuweka ovyo jiwe la kwanza… ".
Watu wanapenda makanisa Parpar zilizo na nafasi safi ya michezo lakini kinacho faa kwetu ni zoezi la Ujumbe moja. Nyuma ya zoezi la Yorodani, waziri Naamani akajifanya kuwa mtumishi wa Elisa, akarejea mara tano akisema kwamba yeye ni mtumishi wa Elisa. Kwa mara ya kwanza huyo mnyonge alitambua kwamba kuna aina mbili ya kuabudu, aina mbili ya makanisa na ya manabii. Kwa shairi la 10, Naamani hakufahamu kwamba yeye ni mdogo kuliko mjumbe wa Elisa lakini sasa amefahamu. Naamani aliona sasa kwamba wafalme, mawaziri, wana-bunge, mamea, wachungaji, mapadre, manabii, wa reverendi, na marais wa dunia walihitaji zoezi la Yorodani. Munaona? Nyuma ya mtu huyo mwenyi mamlaka na mwenyi kiburi, nyuma ya huo utukufu wa bure na utajiri, kulifichama mtoto wa Mungu, mtu mnyenyekevu ambaye jamii iliharibu. Jamii ambayo yenyewe ilijua tu makanisa Parpar na reverendi Gehazi…
Enyi Bwana waziri, wana-bunge, mea, bwana kiongozi, wakati nyinyi mutapata nafasi ya heshima katika kanisa moja, wakati mutakuwa pale kwa kusherehe mwanzo au kushikilia kazi ya kidini, kama munaikubali halafu ukoma wa Naamani ni juu yenu na hapo munahitaji zoezi la Yorodani. Ikiwa munakwenda kanisani kwa kutafuta sauti kwa uchaguzi, kama munatoa zawadi kanisani ili mukubaliwe na watu halafu ukoma wa Naamani ni juu yenu na ni makanisa Parpar, mchungaji wake ni reverend Gehazi. Ikiwa katika kusanyiko mchungaji ana nafasi yake ya upekee hii siyo Yorodani. Je! Iliwezekana kutofautisha Yesu na wafwasi wake? Je! Yuda hakusema: "yule nitakaye mkumbatia, ndiye " je! Mtumishi ni mkuu kuliko mwalimu wake? Watoto wa Ibilisi leo wameketi juu ya mwana punda wa Yesu. Nyinyi, manabii na wasimamizi wa makanisa shukeni na muje kwa Yorodani! Acheni nafasi nzuri nzuri zilizo pwani mwa Parpar na Abana! Ile kanisa ambayo mke wa mtu wa Mungu ameketi pale juu ya mibari, mbele ya kusanyiko, ni Parpar na mchungaji wake ni reverendi Gehazi. Munaona? Mambo haya yanajitokeza kwa wakati wa Ahaba, pamoja na manabii wa Baali na ni Yezebeli ndiye aliwaambia binti zake watende hivi ginsi yeye mwenyewe anavyo kaa kwa kiti cha ufalme wakati Ahaba hayupo. Ni mjukuu wa Yezebeli tu ndiye anaweza kuketi pale, mbele ya wanaume, bila kusumbuka moyoni mwake. Binti za makahaba, wakaidi kama mama zao! Munaona? Kanisa Parpar ndiyo inaweza kufanya hivi na reverendi Gehazi ndiye mchungaji wake. Hii kanisa iliyo na vyombo vya kugeuza hewa, vitambaa udongoni, inayo kubali TV, michezo, kandanda, pwani,… ni Parpar na reverendi Gehazi ndiye mchungaji wake. Hii kanisa ambayo wanawake wamekaa pale wakiwa wamesukwa utambi, wanavaa suruali, wanapaka rangi kwa kucha,… mahali ambapo wanawake wanakuwa kwa sakafu kwa kuhubiri au kuongoza nyimbo, ni Parpar na Gehazi ndiye mchungaji. Hili kanisa ambalo mchungaji ana mercedes kubwa, Patrol, BMW, ni Parpar na Elisa alihubiri kinyume ya mambo haya kwa shairi la 26. Ni watoto wa Gehazi na Elisa aliwahubiri Kelele ya Katikati ya usiku. Kinacho faa kwao ni zoezi la Yorodani. Naamani, waziri wa jeshi alitamani kanisa ambapo simu yake inaweza kulia wakati wa mahubiri, mahali utalii haukatazwe, kanisa sawa na nia yake mahali atabatizwa katika maji safi au kisima cha ubatizo.
Kwa kweli, Naamani alitafuta moja ya hao wachawi katika koti na mabiblia mikononi lakini alianguka juu ya nabii alisi wa Yesu-Kristo.
Munapo kwenda kwa makesha ya maombi ya hao wachawi, hata wewe ni wa kanisa la katholika, protestanti au kiinjili au branhamisti, si kitu, onyesha tu shida zako! Lakini Elisa alilazimisha kwanza zoezi la Yorodani, ndio! Zoezi la Yorodani. Akamuhubiri huyu waziri Kelele ya katikati ya usiku! Mabwana na mabibi waziri, wana-bunge, mea, viongozi, marais,… je! Munataka kuponywa ukoma, saratani, kidonda-ndugu, ukimwi? Shukeni kwanza kwenyi Yorodani! Tafuteni zoezi ya Yorodani! Kama mtu anajidai kuwa mtu wa Mungu na anakubali kuomba anapo kwepa zoezi la Yorodani, yeye ni mchawi! Wakuu wa inchi wanaomba maombi ya hao "manabii" nyumbani mwao kwa siri, zaidi katika chumba ili wapandishwe cheo. Pahali pa mbuzi nyeusi au kuku nyeupe, wanawaomba mafungo na tazameni ginsi gani hao wanao jidai kuwa manabii wananona hakika kama wafumu kijijini, pamoja na nyumba na mitogari za anasa, koti za kimarekani pahali pa ngozi ya kondoo. Je! Siyo manabii, wajumbe wa Mungu, ndio waliwafundisha ninyi kwamba zahabu na feza ni vya Mungu na pia hao hao manabii kwa mfano wa Elia na Yoane mubatizaji walivaa ngozi ya nyama? Munaona? Munahubiri Injili ingine lakini watoto wa Elisa wataikataa!
Je! Nitaacha pori yenye baraka na tulivu ambayo iliona kuzaliwa kwangu na kwenda pumzikoni huko Ulaya? Hapana hata kidogo![…] hatuta kubali hata kidogo msaada, hatuta omba kamwe msaada na usaidizi wa mtu. Hatuta kubali kamwe uhusiano na urafiki wa kanisa fulani. Fanyeni kwanza zoezi la Yorodani! Rais au waziri hawezi kutualika mezani moja nanyi! Hakuna atakaye tualika mezani moja na wakatolika, wabatisti, foursquare, kusanyiko la miungu, pentekoste,… watafute kwanza zoezi la Yorodani!...
Hata kwa ugonjwa wa baba au mama yangu, nitamsaidia kwanza kushuka katika Yorodani. Itakuwa ni uzalimu kwangu kuwaombea ijapokuwa wangali bado wanaomba miungu ya wabatisti, pentekoste, branhamisti, CMA, uamsho, adventisti, katolika, wanaziri, … japo wangali kujiacha kuwekewa mikono na hao wachawi katika koti, [wangali] wanakwenda kwa makesha yao ya maombi. Munaona? Wanapashwa kukata uhusiano na wale wachungaji pia makanisa Parpar. Sina uwezo lakini ni kwa usabitisho wa ujumbe huu Mungu alinipa karama na neema na sitaombea kamwe mtu nje ya ujumbe huu kusudi asizani ni Yesu-Kristo anayeabudiwa kanisani mwake ndiye aliye mponya, ila tu kama ninapata ono. Tutajieleza mbele ya Mungu kuhusu ginsi gani tulitumia yote aliyotupatia.
Naamani alipo ponyeshwa, akafahamu kwamba hakuna Mungu mwingine mbalimbali na yule wa Elisa na kwamba hatakwenda kamwe kusujudu mbele ya [mungu] mwingine. Namna gani nitamwombea mkatolika au mumetodisti ambaye angali anashikamana na mungu wake? Mungu anilinde na mambo haya! Namna gani nitamwombea mtu anaye sema: "kanisa ni kanisa, ni [mungu] moja tu?" Iwe kwa baba yangu, iwe kwa mama yangu, sitaifanya, ila tu kama ni kusudi Mungu awafungue roho kwa kufahamu mambo yale! Na kama sisi ni zaifu, Mungu atusaidie!
Je! Biblia haisemi katika Kumbukumbu la torati 13:1 kwamba kukainuka nabii anaye fanya miujiza au anaye toa ufunuo uliyo haki na baadae anasema: "twendeni kanisani la wabatisti, foursquare, pentekoste, kusanyiko la miungu,… twendeni katika makanisa fulani, misioni au huduma… za miungu wengine", musikwende? Je! Makanisa hizo siyo pahali pa juu sana zinazo tajwa katika 2 Wafalme 17:29-31 na miungu Dagon, Adrammélec, Baali, Rimmon, Baal-Zebub, Kémosh, Moloc,… je! Wote hawaitwi Yesu-Kristo kwa siku hizi? Na Mungu hakutuma ujumbe huu kwa kuwafunua? Je! Biblia haikusema katika Mt.24:24 kwamba kutainuka makristo za uongo toka shimoni? Namna gani mtu anaweza kujidai kuwa nabii (katika kiebrania: nabia= mjumbe) japo hana ujumbe na anaanza kufanya miujiza kwa kusibitisha nini? Namna gani nabii anaweza kuunda kanisa, misioni au huduma kuliko kuleta ujumbe ya uungu? Ni wachawi na wafumu hata kama wao ni katika koti na biblia mikononi. Hakuna wa Elisa wawili wala Yorodani mbili. Wote ni wafumu na mafungo wanao walazimisha ninyi ni picha ya mbuzi nyeusi au kuku nyeupe. Kwa wateule, wa Naamani wa kweli, Biblia ilisema katika Mt.25:6 na Ufunuo 12:14-17 kwamba kutakuja ujumbe na huo ujumbe utawapeleka mbali na udanganyifu… Mbali na makanisa katolika, protestanti, kiinjili, misioni, huduma na ubranhamisti,… mbali na hao manabii wa uwongo. Siku ya hukumu, hamutasema kwamba hamukuharifiwa!
kurudi kwa utaratibu