MAHUBIRI N°18

MASWALI NA MAJIBU (1)


  1/ Ndugu, basi yule asiye kuja kuungama na ambaye hafanyi tena ile zambi ?

    Kama hatendi tena ile zambi, halafu basi ni shetani anaye mdanganya kwani ile zambi moja ni juu yake kama mtu aliyetenda zambi elfu kubwa kubwa. Makosa na laana ni juu yake na juu ya kanisa kwa ajili yake. Haifai tena kushiriki ibada ukiwa na zambi ambayo haikuungamwa. Ni pamoja na zamiri safi na moyo wa furaha ndipo munapashwa kuabudu. Ikiwa kusanyiko ni kubwa, maungamo yamalizike kwanza na kuwe sala moja kwa jumla kwa ajili yao. Zambi zinaweza kuwa zilifanyika kabla kubatizwa, ikiwa zinarudi tena katika mawazo yako, hata zile tulizo zishiriki pamoja na wazazi.

2/ Ndugu Filipo, ni vipi kuhusu anasa ?

Anasa, hata kama haionekani kuwa anasa, inafaa iachwe, hasa [hapa] kwa Kelele ya katikati ya usiku. Mtu moja hawezi kuwa na mamilioni mia ijapo wengine wanatembea kilometre makumi kwa miguu kwa kuja kwa ibada wala hawana chakula. Friji kubwa kubwa, kiti cha bei ghali, pesa katika benki, magari,… koti, karvanti na viatu vya bei ghali, mapambo ya sikio, kantini ya vikwembe, nyumba kubwa kubwa za bei ghali, burudani, utalii, …, [desturi hiyo] inabidi kuiacha ! Mambo yote hayo ndiyo iliyosemwa katika Kelele ya katikati ya usiku pia katika lugha isiyo julikana. Huwezi kuokolewa kama haukutii mambo haya kama vile inavyo semwa katika Biblia na historia, tangu mitume (Mdo.4 :32-37), iliwezekana kwa maakida, matajiri wa aina yote na itakuwa hivyo leo. [Mambo haya] hayawezi kuanguka, niliiona tarehe 24 Aprili 1993. Kumbukeni Marko 10 :17-22 na yule aliye na masikio kwa kusikia asikie.

3/ Ndugu Filipo, ndoa ni kufanya nini ?

Mtu haungi Ndoa kwa sehemu mbili au tatu za kufwatana lakini ni kwa kipindi moja tu. Ni baba ndiye anatoa au anakatalia binti wake kwa ndoa, na sasa mali ya kuoa ndiyo alama moja tu ya ndoa, siyo peta au barua. Ni sherehe ya kutoa mali ndiyo inayo ruhusu ndoa. Na ningependa niseme kwamba siwakataze watu kwenda mbele ya mea wa mji lakini… nataka kusema kwamba ni mamlaka itokayo kwa Mungu kama vile mfalme. Munaona ? Vema! Sasa kama mwanamume anafika pamoja na suria wake au mpenzi mwanamke, wanapashwa mara hapo kuacha kukutana kimwili mpaka wakati mali ya kuoa yatalipwa. Kama mwanamke aliolewa kwa mali maishani mwake na mali haikurudishwa bado, na mume wake angali hai, hawezi kuolewa upya. Ikiwa ulimwoa mwanamke kwa mali na huyo anakwenda kuolewa tena na mume mwingine, yeye anabaki mke wako na watoto anao wazaa kule ni watoto wako hata kama yule mume pia alimwoa kwa mali.

     Kuhusu ndoa, ningependa niseme kwamba watu wawili wanao ishi pamoja pasipo kutoa mali ya kuoa hawaruhusiwi kupokea ubatizo, wote wawili, ila tu kama wanasimamisha tendo yote ya ngono. Lakini kama ni dada peke anaye kuja kwa Bwana, anaweza kubatizwa na kuzidi kuishi katika nyumba ya mume yule ambaye hakulipa mali juu yake. Mume, yeye hawezi kubatizwa kwani yeye ni munyanganyi kama vile inavyoandikwa katika 1Kor.5:11. [Ndl: kwa mach 2006, ndugu Filipo alihubiri juu ya ndoa akisema hivi: "…kwa nyakati za Abrahamu, kulipa mali ilikuwa mwisho wa ndoa lakini Israeli alipo kuwa taifa ambalo lilikuwa na sheria zake zote, wazee wa mji ambao ni mfano wa chumba cha mea walikuwa na sehemu ya ushuhuda katika ndoa na [sisi pia] kwa kawaida tungelipashwa kwenda mbele ya mea ikiwa nchi yetu inge kubali shauri la Kanisa juu ya shauri la Serikali. Mimi kama nabii mjumbe, kama nina vunja ndoa, je! Serikali itakubali kweli? Ni pale kunakuwa tatizo! Munaona? Na ninasonga mbali zaidi kwa kusema kwamba, hata ingawa Serikali ingetembea juu ya msingi wa Biblia sawa Kanisa, sherehe ya urahia ingekuwa ya lazima tu kwa wapagani…"].

4/Ndugu, basi kama mwamini ambaye ilimpasa kuungama anachelewa au hakufika?      

   Kwanza,  alipo tenda zambi, alikutana na mchungaji au alimwita na akamuombea kusudi apewe neema ya Mungu lakini ni kusanyiko ndilo litakalo muombea kwa kweli. Kama mchungaji hakujulisha kusanyiko inafaa kumukumbusha ! kwani mbele ya yote, ni lazima kusanyiko ikuombee, ulikosea Mungu na kusanyiko.

Yule aliye tenda zambi hapaswi kuchelewa wala kukosa kukusanyika lakini kama anafanya hivi, zambi yake isibebeshwe kusanyiko. Kama hafike kwa mara ya pili, wazee watamwendea na kama anafanya kiburi, yeye si ndugu tena. Pia, mashaka na kutokuamini ya mtu haita bebeshwa kusanyiko ikiwa yeye mwenyewe hakuionyesha [wazi]. Kwa maana tunaelekea kwenyi ukamilifu.

5/ Ndugu Filipo, basi kama zambi ilitendwa katika ndoto ? pia ni vipi kuhusu sabato ?

Unapo ona ndoto, inabidi kwanza kutafuta kujua kama inatoka kwa shetani wala kwa Mungu kabla wewe kutafuta tafsiri yake. Lakini, ndoto yote hata ile itokayo kwa shetani inaruhusiwa na Mungu kwa shabaha fulani na kama mara kwa mara  unafanya ngono katika ndoto, halafu kuna zambi za ngono ambazo hazikuungamwa na ni ile pepo ndiyo inakuonyesha zile michezo. Zambi inaweza pia kuwa ya kiroho na kuwa na tafsiri ya kiroho katika mwili. Tunajua kwamba kila zambi inaleta maishani mwetu mapepo [wachafu], ndiyo maana inafaa  kuziungama kwa kufunguliwa toka zile mapepo. Alama zingine zinaambatana na zambi: usingizi katika kusanyiko, ugonjwa unao dumu muda mrefu, kushindwa, na ni kwa Sababu ya zambi ndipo tunakuwa na ibada za timizo. Kama Mungu alikujalia neema uwe mwenye nguvu, funga chakula na uwaombee wazaifu, waimbaji na wahubiri. Inafaa waimbaji wawe na utayari ili wasije hapa  kwa timizo, lakini kwa kuwatia watu katika Roho na kumupa Mungu ibada ambayo ndani mwake kuna hata ubatizo wa Roho-Mtakatifu, ufungulifu, …kuabudu kama mtindo wa zamani. Kitu ambacho vidari na vyama vya mziki haviwezi kutoa. Tumaini ni juu yao na hawawezi kuisaliti. Mwimbaji akikaribia mazabahu wakati yeye ni mchafu, ni adui kwetu, anaye tafuta kifo chetu.

      Kuhusu sabato, tunapata waadventista wa siku ya 7 katika Mt. 12:1-8 pia Yne 9 :16 wakimusukuma Yesu kushika sabato lakini aliwaambia: mimi ni bwana wa sabato. Ni pepo ya kale. Juma mosi ikawa sabato ya agano la kale katika damu ya mabeberu na ya ngombe dume lakini juma pili ikawa sabato ya agano jipya katika damu ya Yesu. Eb.8:6-8, 1Kor.11:25. Biblia inatuambia kwamba ni jumapili ndipo walikuwa wakikusanyika: 1Kor.16:1-2, Mdo.20:7,…kaizari Constantin alifanya tu juma pili kuwa siku ya pumziko wakati yeye mwenyewe aliongoka. Na ilikuwa kupitia amri kwa mwaka 327. Paulo pia aliwahamakia hao wanao fwata sheria katika Gal.4:9-10. Katika Kol.2:16, Paulo anasema: mtu asiwahukumu kuhusu sherehe, mwezi kuandama au sabato ambavyo ni kivuli cha mambo yatakayo kuja…

 6/ Kama inavyo andikwa katika Marko 13:35, kwa wakati gani twaweza kuweka kuchukuliwa?

    … Wewe uliye mubranhamisti, kama kuchukuliwa inapaswa kufanyika katikati ya usiku au jogoo inapowika au asubuhi, kwa nini unashughulika? Kama kuchukuliwa itafanyika katikati ya usiku, basi utafanya nini? Kama unataka kuijua, nenda uchunguze vitabu vya William Branham! Kama tu hamuja wai kuachana na matengano zenu na kuja hapa kwa unyenyekevu, munapo niomba maji ya kunywa nitawapa siki. Siyo swali ambalo ulipaswa kuniuliza… hukumuni, inafaa umwambie Mungu kwamba hukuamini kwa sababu nilikuwa na majivuno sana duniani.  [Ndl. : ilikuwa wakati wa mahubiri hazarani].

7/ Ndugu Filipo, ni wakati gani karama zinapashwa kuanza kutenda?

Kabla, wakati, na baada ya ibada kwa kila pumziko ndogo, hasa kunapo kuwa kimia kwa wakati fupi lakini hapana wakati wa mahubiri ambayo pia ni tukio la Roho. Wakati wa mahubiri kunapaswa kuwa heshima kamilifu ; kusiwe ma « Amina ! » pasipo utaratibu, kusiwe ma « Hubiri ! Sema yote ! », hakuna michezo ya kupendeza macho au maburudisho, kusiwe kila kuhisi ya ubinadamu. Wakati wa maombi, fungeni macho ili musizubae na mujiweke tayari mikononi mwa Roho mtakatifu. Lakini kama munafanya ufungulifu, fungueni macho. Kusanyiko inafunga macho ili wasizubae wala kupokea pepo aliye fukuzwa. Lakini shemashi anabaki macho wazi. Basi ibada inaanza na maungamo mbele ya kusanyiko pia baada ya mahubiri, kuombea wagonjwa pia ufungulifu na lengo zingine. Pia, wakati wa maombi ya ukimia, inabidi kujingojea kwa karama za Roho.

8/ [Swali hilo liliulizwa wakati wa nafasi kwa maswali na majibu baada ya mahubiri ya ndugu Filipo alipo alikwa katika kusanyiko la ujumbe wa jioni, tarehe 04 septemba 2005 huko Abidjan. Aliye pewa kusema anasoma katika kijitabu cha William Branham na anaanza…] "Bwana Filipo…, tunabariki Mungu aliye tuangaza kwa mjumbe wake William Marrion Branham kuhusu Kelele ya katikati ya usiku. Ndugu Branham alitutoa gizani kwa kutuongoza hadi nuru na sijui unataka kutuelekeza wapi na ninaonyesha kwamba hii Kelele ya katikati ya usiku ni vema tu kwa yule asiye jua Ujumbe ya ndugu Branham kwa sababu yote umeyasema tayari inapatikana katika brosha za ndugu Branham, ninakupigia asante!”

     [Ndl: Ndugu Filipo anajibu…] Ninafurahi ee ndugu ginsi Ujumbe wangu ni ndani, hasa kwa usawa wa ujumbe ya William Branham ambaye yeye mwenyewe alisema: nilihubiri ujumbe moja kama Paulo. [Yule aliye pewa neno anasema: "si sawa!" Ndugu Filipo anaendelea…]. Na kuhusu kwenda kwa nuru, ni kama Yesu aliye kuwa akialika wafarisayo kwa uhuru na hao walikuwa wakimwambia Yesu:… tuisome: « wakamjibu: sisi ni uzao wa Abrahamu, na kamwe hatukuwa utumwani mwa mtu yeyote; namna gani wewe unasema: mutawekwa  huru ? » munaona? Kwa mawazo yao, tayari Musa amewatoa utumwani mwa Misri, ni mwisho! Na Luteri alipo watoa watu gizani, ni nani aliyewarudisha tena gizani kusudi Mungu atume Wesley? Na ni nani aliye warudisha wametodisti gizani kusudi Mungu atume William Branham? Na kama madhehebu wangemwambia Branham kwamba hawahitaji nuru kwa maana Paulo alisema katika Efe.5:8, " kwa maana zamani ninyi mulikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana…" na Paulo anasema tena katika 1Tes.5:5: « kwa maana ninyi wote ni wana wa nuru na wana wa mchana; sisi si watu wa usiku wala watu wa giza». Mungelisema basi nini -? [na mwingine akakamata neno siku ile ile:..]= "katika mahubiri yote, ulikuwa ukituita wabranhamisti. Ningependa urekebishe maneno yale kwani sisi si wabranhamisti lakini sisi ni wakristo. Kuna wabranhamisti na hao hubatiza au kuomba kwa jina la Branham lakini sisi si wabranhamisti, rekebisha masemi yale!". [Ndugu Filipo anajibu:…]

      Ndugu, ningependa nikuambie kwamba wale wanaoitwa waluteri hawabatizi kwa jina la Luteri. Tangu walipo kataa ujumbe wa Kalvini, wakubali au wakatae wao ni waluteri. Hawakutaka waitwe hivi lakini watoto wao walikubali baadae. Leo hii mumefanya "ndugu wa ujumbe" kuwa jina lenu, siku inayo kuja watoto wenu wataitwa wabranhamisti pasipo kujua. Mubatize au muombe katika jina la Branham, muwe wenye kuamini ngurumo, wasiyoamini ngurumo, wafrankist, wenyi kushika sheria, wanao amini neema au haizuru nini, ni maelezo tu. Ninyi wote ni wabranhamisti! Kuna aina makumi ya wabatisti na wale wanao batiza katika jina la Branham ni aina moja tu ya wabranhamisti. Hata kati ya wale wanao amini ngurumo, kuna matawi: wanao hubiri ngurumo za ufundi, wanao hubiri ngurumo zenyi nguvu, na vivi hivi. Na sasa tunapokuwa katikati ya usiku ikiwa imani yako inasimamia mambo iliyo semwa na William Branham au ujanja wa Ewald Frank au anaye jidai kuwa [sijui] kitu gani, ninyi wote ni wabranhamisti, mukipenda wala musipomenda. Tangu wakati mtu yuko katika kanisa katolika, ni zambi kwangu mimi kumwita mkristo. Na namna gani anaweza kuniambia: "usiniite mkatolika!". 

      [kukawa na ghasia kuu siku ile lakini neema ya Mungu ikashinda na tangu siku ya kwanza tarehe 05 Septemba hadi jumapili tarehe 11, kusanyiko nzima hata mchungaji na msaidizi wake wakaamini na wakabatizwa upya. Na yule aliye jitwalia masemi yeye pia akaamini na akabatizwa].

9/ Ndugu Filipo, tangu tarehe 24 aprili 1993 hadi tarehe 8 julai 2002  ulikuwa na kazi gani kwa kanisa la ubatisti hadi wakati wa jioni?

Ndugu, sikuwa nayo hata moja! Kila mara ninakuwa tu mwaminifu wa kawaida. Hadi machi 2002 wakati ambapo nilipokea amri ya kuhubiri, nilikuwa kama mtu anaye kwenda kanisani kwa mara ya kwanza. Mimi ni mwembamba kama mtume Paulo [Ndl: 2 Kor.10:1] hasa maskini, namna gani naweza kuwa kitu [cha maana]    kati yao? Mtu asiye na elimu kubwa,… Tangu 1992 hadi 1993, nilikuwa msaidizi  wa wajenzi kwa kazi ya majengo. Nilikuwa nikiwabebea sementi wafundi wa majengo. Walikuwa waghana na watogo. Basi namna gani ningeweza kuwa kitu [cha maana]? Tarehe 27 Mei 1997 niliandika kwa ukurasa wa kwanza wa Biblia hii,… nitaisoma: "Baba mpendwa, ninakuandikia barua hii kwa kukujulisha imani yangu katika muda nitakao fanya hapa ninapo kungojea mpaka utakapo kuja kunitafuta kwa kurudi nyumbani… Baba, mapenzi yako yatimizwe na hapana ya kwangu… na kama moyo wangu unanipa nguvu njiani mwa upotevu, utumie neema yako kwangu hata mkono wako wa kuume unirudishe kwani mimi si mmoja wa wale wenye hekima wala wanao weza kuvumilia hasira yako… singependa nifanye kitu; napenda kungojea kuja kwako katika ukimia. Ndiyo, katika ukimia. Amina! Kuja Bwana Yesu, napenda nirudi nyumbani.". Munaona? Aliye wa Mungu, Mungu anajua kumungojesha. Leo watu wanapoona jambo moja mara hapo wanajiingiza katika mavuno. Sio tu maneno yale lakini kila mara ninangojea kupokea kitu fulani kutoka kwa Mungu na kusukumwa kuyahubiri kabla niyahubiri ndio maana sija wai kusahihisha mafundisho hata moja. Sija wai kufanya utafiti juu ya siri zilizo katika Biblia. Sikusema kamwe: "Ee Mungu unipe mwangaza juu ya siri fulani!". Mtumwa mwema anabaki kimia na kungoja kwa bwana wake. Mahali Yesu alikuwa kati ya miaka kumi na miwili hadi miaka makumi tatu, ni pale nilikuwa tangu 1993 mpaka 2002.

10/ Ndugu Filipo, mtu mmoja anasema kwamba Ufu.10:7 haisemeki juu ya ndugu Branham? Je! Ni kweli?

    Siku zijazo, sitapoteza muda wangu kwa kujibu swali kama hilo… Baada ya nyakati za jioni, nabii gani alitumwa na Mungu kwa kusema maneno yale? Ndugu, kama ni kweli halafu William Branham ni nabii wa uwongo na wote walio tumwa naye ni waongo hata Ewald Frank. Katika siku zote za huduma yake, alitegemea hii shairi na alifunua mihuri saba na yote tunayoijua kwa nguvu ya Ufu.10:7. Wandugu, ninyi ni huru kula mutakacho lakini siwezi kujiachilia kuzubaishwa na onyesho la mteolojia mdogo aliye mumetodisti ambaye yeye mwenyewe aliangazwa kwa ujumbe ya William Branham. Siamini huduma ya usahihisho wa nabii. Yoane mubatizaji aliposema yeye ni Isaya 40:3, sifahamu namna gani Yesu ambaye alionyeshwa naye anaweza kuja kusema kwamba Yoane siye Isaya 40:3. Na Yesu anaposema yeye ni Isaya 61, sielewi namna gani Paulo au Petro ambao walionyeshwa naye wanaweza kuja kusema kwamba Yesu siye Isaya 61. Namna gani Timoteo anaweza kuja na kusema kwamba Paulo siye Isaya 49:6 na nyinyi mutamusikiliza? [ Ndl: Mungu alionyesha katika mahubiri: "maono ya mto Kebari na ya Patemo" kwamba nyota ya saba ya ufunuo 1:16 na malaika wa saba mwenyi baragumu na malaika wa saba mwenyi kikombe na malaika wa saba wa Laodikia alikuwa ni malaika mmoja tu akibadilisha huduma].

11/ Ndugu Filipo, twapahswa kufanya nini tunapo fukuzwa wakati wa mahubiri hazarani?

   Ndiyo, nasikia ikisemeka kwamba wandugu hawarudi nyuma wakiwa mbele ya mateso. Wandugu, hatuhubiri Injili tofauti na ile ya Yesu. Imesemwa katika Mt…. «Na tazama mji yote ikatoka na kuja mbele ya Yes ; na walipo muona, wakamusihi aende zake mbali na mji wao. Na alipo panda katika chombo, akapita ngambo ingine ya maji, na kuja katika mji wake mwenyewe.». Ingine mwandiko wa Yoane inasema: «wakatwaa mawe ili wamtupie ; lakini Yesu akafichama na kutoka hekaluni». Mateso itakuja watakapo tufungia kuhubiri ujumbe huu. Mujue basi kuhepuka vizuio kwani njia ni ndefu. Wakiwafukuza ngambo hii, piteni ngambo ingine ya maji! Na munapo toka kwa kuhubiri, muwe watu wawili au watatu.

12/ Ndugu Filipo, ninapo tamani kumfanyia Mungu kitu fulani duniani na nisipo weza kuhubiri wala…, nili mtolea zawadi mchungaji niliye muwazia kuwa mtumishi wa Mungu. Je! Naweza kwenda kuomba nirudishiwe?

   Hapana dada! Mtu haombi kurudishiwa zawadi [aliyo itoa] ila tu kama ni uwanja au nyumba, ikiwezekana. Lakini sitapenda mtu arudilie nyumba au uwanja kwa kuitoa [baadae] zawadi katika ujumbe huu. Munaona? Ni hivi! Dada, ni jambo la kujuta lakini nafurahishwa na nia yako. Ilikuwa pia hivi kwa Maria wa Magdala, Suzana na wengine wengi kando ya Yesu.


Tuma ukurasa huu kwa rafiki

kurudi kwa utaratibu

www.matth25v6.org - Copyright © Aprili 2007
Kisheria Deposit ® All rights reserved